today news

VIONGOZI WA BAVICHA WAKAMATWA DODOMA

Viongozi sita wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) wamekamatwa na Polisi mjini Dodoma kwa madai ya kukusudia kuikashifu Serikali.

Katika siku za karibuni, viongozi wa Bavicha wamekuwa wakitoa matamko mbalimbali ya kuwahamasisha wafuasi wake kuja mjini hapa kwa kile walichoeleza kuwa ni kuisaidia polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM uliopangwa kufanyika Julai 23 kwa madai kuwa jeshi hilo lilishapiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Hata hivyo, jana polisi imetoa ufafanuzi juu ya kauli yake ikisema kwamba kilichozuiwa ni mikutano ya hadhara ya siasa na siyo ya ndani kama huo wa CCM..

Awali polisi waliwakamata Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya, George Tito, Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeye na Katibu Bavicha Wilaya ya Temeke, Hilda Newton na baadaye Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema, Joseph Kasambala aliyekamatwa baada ya kwenda kituo cha polisi kwa lengo la kuwawekea dhamana wenzake.


Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa

Usipitwe!! kupitia FACEBOOKTWITTER naINSTAGRAM kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..!! Usiache ku download application play store BOFYA HAPA KU DOWNLOAD....... LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOKLIKE PAGE 

DOWNLOAD APP YA "BONGOHOTZ" UPATE NOTIFICATION KWA KILA KITU KIPYA 

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI

Post a Comment

Post a Comment