Wachezaji mpira wa miguu ni watu ambao
wamekuwa wakimiliki fedha nyingi kutokana na kulipwa mishahara mikubwa
kwa wiki, ni kitu cha kawaida kwa mchezaji mpira kulipwa pound 100,000/=
kwa wiki ina maana kwa mwezi analipwa pound 400,000/= ni zaidi ya
bilioni moja ya kitanzania.
Hivyo wengi wao huwa wanaishi maisha ya juu kulingana na mishahara yao wanayolipwa, kwa mujibu wa mtandao wa therichest.com
mwishoni mwa mwaka 2014 walitoa list ya nyumba kumi za gharama
zinazomilikiwa na mastaa wa soka wanaocheza soka katika nchi tofauti
tofauti.
10. Nahodha na mshambuliaji kutoka Argentina Lionel Messi
ameingia katika hii list na nyumba yake imepewa namba 10 licha ya
thamani yake halisi kutokuwa hadharani, lakini inatajwa kuwa moja kati
ya nyumba 10 za thamani, ipo katika mji wa Barcelona mji ambao klabu yake ndio ilipo FC Barcelona.
9. Ricardo Kaka huyu ni staa kutoka Brazil lakini pia amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’or mwaka 2007 akiwa katika klabu ya AC Milan ya Italia wakati huo lakini kwa sasa anaichezea klabu ya Orlando City. Kaka anaingia katika hii List nyumba yake ina thamani ya dola milioni 3.
8. Andres Iniesta
huyu ni moja kati ya wachezaji bora duniani wenye uwezo wa kucheza kwa
ufasahaa nafasi ya kiungo lakini bado ni moja kati ya viungo wa
kutegemewa katika klabu ya FC Barcelona, Iniesta ni moja kati ya wachezaji wanaomiliki nyumba za kifahari. Nyumba yake ina thamani ya dola milioni 4.6.
7. Mario Balotelli huyu ni muitaliano mwenye asili ya kutoka Ghana
kwa baba na mama, amekuwa maarufu kutokana na uwezo wake uwanjani
pamoja vituko vyake ila hayupo nyuma katika masuala ya kumiliki nyumba
za thamani, nyumba yake ina thamani ya dola milioni 4.86.
6. Cristiano Ronaldo huyu ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or anaitumikia klabu ya Real Madrid ya Hispania
kwa sasa lakini ni mtu ambaye anamiliki nyumba nyingi za thamani ila
hii ni moja kati ya nyumba anazomiliki na inathamani ya dola milioni 6.
5. Frank Lampard amewahi kutamba katika klabu ya Chelsea ya Uingereza na timu yake ya taifa ya Uingereza kabla ya hivi karibuni kuamua kwenda kumalizia soka lake katika klabu ya New York City ya Marekani. Lampard ana nyumba yenye thamani ya dola milioni 7.
4. John Terry ni nahodha wa klabu ya Chelsea
lakini ni moja kati ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya
Uingereza anamiliki jumba lenye thamani ya pound milioni 7.5.
3. Didier Drogba ndio mchezaji pekee kutoka Afrika aliyeingia katika top ten hii huyu ni staa aliyecheza katika klabu ya Chelsea kwa mafanikio kwani hadi leo yupo katika kumbukumbu ya wachezaji wenye heshima katika klabu ya Chelsea. Drogba ana nyumba yenye thamani ya dola milioni 9.
2. Wayne Rooney ni nahodha wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, ni mtu anayeongoza safu ya ushambuliaji kwa klabu ya Man United, anamiliki jumba lenye thamani ya dola 17.83.
1.David Beckham hadi anastafu kucheza soka alikuwa anatajwa kuwa mchezaji tajiri duniani, Beckham amejipatia umaarufu akiwa katika klabu mbalimbali ikiwemo Manchester United kutokana na umahiri wake wa kufunga magoli kwa kupiga faulo. Beckham anamiliki jumba lenye thamani ya dola milioni 20.
Post a Comment