Imelda Mtema
FAIZA Ally, ambaye ni mzazi mwenzie na mbunge wa Mbeya mjini kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Mr. Sugu’ anadaiwa kukata rufaa na kurudi mahakamani kudai upya haki yake juu ya malezi ya mtoto wake.
Mrembo huyo mwenye vituko kwenye suala la uvaaji ‘alitinga’ mahakamani hapo sanjari na mwanasheria wake, ndugu na baadhi ya watu wa karibu kwa lengo la kupinga hukumu iliyotolewa awali katika Mahakama ya Mwanzo ya Sinza jijini Dar, iliyoamua kuwa hana haki ya kuishi na mwanaye (Sasha).
Hata hivyo, Faiza alikataa kuzungumzia suala hilo, kwa kile alichokiita… “suala liko mahakamani, tuiachie uhuru wake”. Kesi hiyo itaanza kuunguruma upya mnamo Agosti 18, mwaka huu.
Post a Comment