MTANGAZAJI wa Kipindi cha Harusini kinachorushwa kupitia DSTV, Pennieli Mungilwa amefunguka kuumizwa na uzushi unaosambaa kuwa amenasa ujauzito kitu ambacho kinahatarisha uhusiano wake wa kimapenzi.
Akizungumza na Star Mix, Penny alisema kuwa, jambo la mimba ni la heri lakini lazima lisemwe kwa ukweli siyo kuzusha kwa sababu linaleta matatizo makubwa sana kwa mtu ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine.
“Yaani sina ujauzito wa mtu yeyote yule na hakuna mtu mbaye hapendi kupata lakini kwa mtu sahihi na wakati muafaka sasa mimi watu wakinibambika hilo wananiletea shida pia kwenye uhusiano wangu nilionao,” alisema Penny.
Post a Comment