bongohotz

SABABU ZA MUWASHO SEHEMU ZA SIRI KWA MWANAUME NA MWANAMKE NIMEKUWEKEA HAPA -Bongohotz.com

Hizi sababu na tiba ya muwasho Sehemu za siri
KUWASHWA sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani kujumuisha maradhi ya uke kwa wanawake au muwasho na kuvimba kwa sehemu za siri za wanaume (jock itch).

Bila kujali jinsia muwasho unaweza kusababishwa na ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya zinaa au mzio (allery). Kuwashwa makalioni hutokea pale ngozi inayozunguka njia ya haja kubwa inapokereketa ikiambatana na hamu ya kutaka kupakuna, muwasho huongezeka pale unapokaa na kukiwa na unyevunyevu. Aidha, sababu kuu za kuwashwa kwenye makalio ni kutojisafisha vizuri, kula vyakula vyenye viungo vingi sana, kuhara, vidonda kwenye njia ya haja kubwa, maambukizi ya fangasi, bawasiri (hemorrhoids), minyoo na kadhalika.

Watu wengi wakiwemo wasomaji wa Bongohotz.com wamekuwa na tatizo la muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu flani na huisha wenyewe baada ya kitu hicho kikiondolewa, vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi, ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.

Nini husababisha muwasho sehemu za siri za Mwanaume?
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu zingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa, mzio, maambukizi ya bakteria n.k
Nini hupelekea muwasho wa sehemu za siri kwa Mwanamke?
(i) Maambukizi ya Fangasi Ukeni (Vaginal Yeast Infection), Ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni uwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

(ii) Ugonjwa wa kuvimba uke (Vulvovaginitis), Ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.
(iii) Kuvimba Uke baada ya hedhi kukoma (Postmenopausal Atrophic Vaginitis), Ni ugonjwa wa kuvimba kwa uke baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

TOA MAONI YAKO NA SHARE KUPITIA WHATSAPP, FACEBOOK NA TWITTER.

Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usiache ku download application play store kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..Karibu

DOWNLOAD APPLICATION HAPA..!!


LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK
Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Post a Comment

Post a Comment