WAZIRI KIJAJI AWASILISHA TAARIFA YA KIWANDA CHA 'TANZANIA BIOTECH PRODUCTS-TBPL' KWA KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA - Swahili Viuhapa
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali itaendelea kuliwezesha Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za umma katika uzalishaji na usambazaji wa viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria ili kutokomeza ugonjwa huo nchini.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati wa utoaji wa Taarifa ya Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi waenezao ugonjwa wa malaria (Tanzania Biotech Products – TBPL) kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 4, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) amesema Kamati hiyo imedhamiria kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini na iko tayali kushirikiana na Wizara kuona Shirika hilo linafanya kazi kwa ufanisi katika kuzalisha viuadudu hivyo na kusambaza nchi nzima ili kuokoa maisha ya watanzania wengi.
Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha uzalishaji na kuweka utaratibu mzuri wa ununuzi na usambazaji wa viuwadudu vinanvyouwa viluwiluwi wa mbu waenezao malaria ili kutokomeza malaria nchini katika kipindi kitakachopangwa .
Awali, akitoa taarifa hiyo ya Kiwanda cha TBPL kwa wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Dkt. Nicholas Shombe amesema Serikali imeanzisha Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi vya mbu waenezao Malaria na magonjwa mengine Dengue, Zika, Chikungunya, Matende na Mabusha ili kutokomeza magojwa hayo nchini.
Kiwanda hiki cha TBPL kilichopo mkoani Pwani, kinamilikiwa na Serikali kwa 100% chini ya NDC na una uwezo wa kuzalisha Viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu,
viuatilifu vya kibalojia ( bio – pestcides) kwa ajili ya kuua wadudu wadhurifu katika mazao ya pamba na mbogamboga na mbolea (bio – fertilizer). Kwa mujibu watakwimu za NBS 2020, Dawa hizi viuadudu zimechangia kushuka kwa maambukizi ya malaria nchini kutoa asolkmia 14 hadi 7.3. Amesema Dkt. Nicholas Shombe.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akitoa majumuisho ya maoni na mapendekezo ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa utoaji wa Taarifa ya Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi waenezao ugonjwa wa malaria (Tanzania Biotech Products – TBPL) Februari 4, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) akiongoza kikao cha utoaji wa Taarifa ya Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi waenezao ugonjwa wa malaria (Tanzania Biotech Products – TBPL) kwa Kamati hiyo Februari 4, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili
soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.
Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb
The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.
Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania
Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.
vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.
Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.
https://www.swahili.viuhapa.com/waziri-kijaji-awasilisha-taarifa-ya-kiwanda-cha-tanzania-biotech-products-tbpl-kwa-kamati-ya-bunge-ya-kudumu-ya-viwandabiashara-na-mazingira-swahili-viuhapa/
Post a Comment