stories

CHOMBEZO: SLAVE SEX...MTUMWA WA NGONO..(SEHEMU YA 6)


SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)....(6)
AGE….(18+)

ILIPOISHIA
“Embu nipatie namba yake ili niweze kufanya naye mazungumzo mimi mwenyewe, kuna kazi tayari nishamtafutia anatakiwa kuanza kesho,nitajie namba zake za simu”
Hakuna siku aliyokuwa katika wakati mgumu kama siku hiyo,Nickson alikuwa akijishauri kichwani ni kitu gani akifanye.
SONGA NAYO.
Kichwani mwa Nickson alielewa jambo moja tu, hakukuwa na kazi yoyote hapo, isipokuwa bosi wake anamtaka Mke wake Gloria kimapenzi,hilo alilielewa wazi baada ya kuunga matukio, aliumia zaidi hasa alipomfikiria mke wake alivyokuwa mzuri,alimeza mate huku akifatakari ni jambo gani alifanye,kitendo cha kutotoa namba za simu kilimaanisha kumuweka katika uhusiano mbaya na Mzee Magugu bosi wake, aliyekuwa nyuma ya meza anamsisitiza atoe namba huku akizugusha kiti chake.
“Hizi hapa bosi”
Alisema Nickson huku akimuwekea bosi wake simu mbele yake, ambapo tayari aliweka jina lilioandikwa ‘my lovely wife’ juu ya tarakimu.
Mzee Magugu hakuchelewa hapohapo alizichukua na kuanza kuzipiga ili kumtoa Nickson wasiwasi, akaweka ‘loudspika’haikuchkua hata sekunde tano upande wa pili wa simu ukapokelewa.
“Mama Shayo,hujambo?”
“Sijambo nani mwenzangu?”
“Oh rafiki yako mimi, umenisahau?”
“Usinipotezee wakati,huna jina?”
“Ah sasa mbona mkali?”
“Nina kazi za kufanya,kama huna cha maana usinisumbue”
Gloria aliongea kwa ukali kidogo,Mzee Magugu akajichekesha.
“Nipo na Mumeo hapa”
“Nickson?”
“Ndio huyo huyo”
“sasa ndiyo useme ivyo,hajambo kwanza mume wangu?”
“Hajambo sana,naona mpaka kanenepa ana kitambi,unampikia nini?”
“Chakula cha kawaida tu,mpo wapi kwanza?”
“Tupo ofisini hapa,ushanikumbuka mimi?”
“Hapana”
“Mlikuja kunipokea Airpot jana,mimi ni bosi wake”
Kusikia hivyo, Gloria hakujibu kitu kingine kwa karibu sekunde nane.
“Halloo Mama Shayo”
“Abee”
“Mbona kimnya?”
“Amna kitu”
“Sasa… nilikuwa nakwambia zile habari za kazi,nishakutafutia tayari na unatakiwa kesho uanze mara moja,ivyo uje hapa na Nickson ili nikupe utaratibu”
“Aya”
Maongezi kwa njia ya simu yakaishia hapo na simu ikakatwa, Moyoni mwa Mzee Magugu alishaapia kuwa, ilikuwa ni lazima amjaze Gloria kingi,na ni kweli mpaka hatua aliyofikia alijipa moyo,mbali na kuwa bosi wa Nickson Mzee Magugu alikuwa ana uwezo kifedha, hiyo ilimpa moyo zaidi!
Alimruhusu Nickson akaendelee na kazi huku akizidi kuvuta picha ya Gloria kichwani kwake.
Japokuwa msichana huyo alikuwa mchaga lakini alikuwa ana makalio kiasi na kufanya nyuma abinuke hiyo ndiyo ikamtia hamasa zaidi.
“Huyu mtoto lazima nimpate kwa gharama yoyote ile,Nickson hawezi kumiliki mke mzuri kuliko wa bosi wake,kwa kipi alichokuwa nacho”
Hayo yalimiminika ndani ya ubongo wa Mzee Magugu huku mara kadhaa sura ya Gloria ikipita kichwani kwake kama mtu anaye angalia sinema!
****
Nyumbani kwa Nickson kulizuka ugomvi mkubwa sana,kitendo cha Nickson kutoa namba za Gloria ndicho kilifanya nyumba nzima ijae kelele usiku huo wa saa mbili baada ya Nickson kutia maguu!
“Mimi sijapenda,nimekwambia sitaki kazi zenu,au unataka kuniuza kwa bosi wako?sema kabisa,nambie kama mna njama,maana sikuelewi,mimi nimekwambia nini kinaendelea wewe hutaki kunielewa,unachotaka nini sasa?unaomba msamaha wa nini?unaomba msamaha wa nini? wakati ushatoa namba,kwa kweli umenikera Nick,umeniudhi sana,niache usinishike,usinishike.. niache nakwambia”
“Gloria naomba unisikilize”
“Siwezi kukusikiliza tena,inaonesha ni kiasi gani una nidharau”
“Yule ni bosi wangu”
“Kwahiyo?”
“Ningekataa isingekuwa picha nzuri”
“Picha nzuri eeeeh!wewe si unamuogopa,mimi namtukana akianza kunieleza upuuzi wake”
“Utakuwa unakosea,utaniweka kwenye matatizo”
“Matatizo gani?”
“Yule ni bosi wangu,kumbuka ndiye ananilipa”
“Ndiyo maana hauna msimamo,labda umuwahi umwambie kuwa asinipigie lakini vinginevyo,ataipata freshi”
Gloria alikuwa katika hali ya ukali na kukasirishwa sana mpaka rangi yake ya mwili ikabadilika na kuwa nyekundu, mishipa ya shingo ilimtoka na Nickson akaogopa,
hakuwahi kumuona Mke wake akiwa katika hali kama hiyo hata siku moja,hiyo ilimchanganya akili,seblen pakawa hapakaliki tena.
Haikupita hata sekunde tisa ukimnya ukatawala baada ya simu ya Gloria kuita na Nickson alivyotambua kuwa anayepiga ni bosi wake akamkazia macho Gloria ambaye alikuwa keshaipokea simu na kuiweka ‘loudspika’ ili Nickson asikie.
“Ooh Mrembo”
Hiyo ndiyo sauti iliyosikika seble nzima baada ya kupokelewa.
“Abee”
“Sasa hivi unafanya nini?”
“Nipo na Mume wangu”
“Napenda sana ndiyo wakati wake huu,maana najua amechoka, inabidi umkande kidogo,si unajua tena”
“Naelewa”
“Vipi kuhusu kesho?”
“Kuhusu nini?”
Gloria alijibu kifupi kwa mkato.
“Tulivyoongea Mchana,Nickson hajakueleza?”
“Kanieleza lakini sipo tayari”
“Sasa kwanini?au Nickson ndiyo kakukataza?”
“Mimi ndiye nimekataa”
“Mpe simu Nickson”
Nickson akasogezewa simu.
“Halloo bosi”
“Habari za jioni?”
“Salama tu sijui huko?”
“Sasa mbona umemkataza mkeo kuja kufanya kazi?”
“Siwezi kufanya ivyo,yeye mwenyewe hataki”
“Umemkataza bwana usibishe!”
Mzee Magugu akaongea kwa sauti ya ukali kidogo.
“Siwezi bosi, nilijaribu kumwam…”
“Okay”
Hapo hapo simu ikakatwa, hiyo ilimtia mashaka Nickson, alishaelewa ni kiasi gani bosi wake amekasirika,alishusha pumzi na kumtizama mkewe kwa macho ya huruma.
Moyoni aliumia mno na alijiurumia sana,kukataa kazi kwa Gloria kulimfanya auzunike sana, alishaelewa kuwa yupo mbioni kufukuzwa kazi.Alishika tama huku akiwa mwenye mawazo.Gloria alivyomuona Mme wake katika hali hiyo alisikitika zaidi na kuguswa.
“Nickson”
“Naam Mke wangu”
“Una waza nini?”
“Sio kitu mke wangu”
“Nakupenda,nakupenda sana lakini sipo tayari kuona ndoa yangu inaingia kwenye matatizo,hiyo kazi sipo tayari naomba unisamehe”
Nickson alielewa wazi kabisa kuwa Gloria hatanii na alikuwa ni msichana mwenye msimamo mno pengine kuliko yoyote Yule aliyewahi kuwa naye kabla!
Kivyovyote vile hata kama angeendelea kumsihi kuhusu kukubali kazi ingekuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa! Nickson siku hiyo hakula chakula kabisa na hata alivyofika kitandani hakuwa na hamu na tunda la mke wake, kifupi hakuwa katika Mudi!
*****
Mambo hayakuishia nyumbani tu, ilikuwa ni kama alitabiri, kwani alipofika ofisini siku hiyo hawakuongeleshana na Bosi wake na ilipofika majira ya saa saba mchana muda wa kwenda kula Nickson alisimama kuelekea nje na alivyofika mlangoni alikutana na Bosi wake akiwa ameukunja uso wake na kuonesha kuchukizwa baada ya kumuona Nickson mbele yake.
“Nifate ofisini”
Mzee Magugu alisema bila ya kumuangalia Nickson usoni kisha kumpa mgongo akiongoza mbele.
“Sawa bosi,lakini naenda kula mara moja”
Mzee Magugu aligeuka ghafla akiwa ameukunja uso wake huku macho yake yakionesha hasira na chuki.
“Tangu lini umeanza utovu wa nidhamu?mimi nakuita ofisini kwangu unasema unaenda kula!”
Mzee Magugu alifoka na sauti yake nzito kuenea ofisi nzima!

ITAENDELEA.....toa comment yako kisha share kwa wengine. SOMA CHOMBEZO LA SLAVE SEX NO 5 KWA KU BOFYA HAPA


TOA MAONI YAKO HAPA BONGOHOT