Ili mtu aweze kufanikiwa malengo yake anapaswa kuwa na mahitaji fulani. Moja ya hitaji kubwa na la msingi ni kuwa na afya njema. Endapo mtu hatakuwa na afya njema atatumia gharama kubwa na muda mwingi ili kuboresha afya yake.
Zifuatazo ni funguo tano za kudumisha afya njema
Zingatia Usafi
Mtu kuwa na afya bora inabidi kuzingatia usafi wa mwili, mazingira anayoishi pamoja na vile anavyokula na kunywa. Kuna magonjwa mengi yanasababishwa na mazingira machafu, kwa mfano magonjwa ya kuhara na mchochota wa ini. Kudumisha usafi kunaweza pia kuepusha kuenea kwa magonjwa hatari kama vile nimonia (kichomi) na magonjwa ya kuhara.
Pata mlo kamili na unaofaa
Ili mtu awe na afya nzuri, anahitaji chakula chenye lishe bora. Mtu anahitaji kula vyakula vya kujenga mwili, kuupa mwili nguvu na kulinda mwili. Hivyo unapokula tumia pia matunda, mboga na uwe na kawaida ya kula vyakula vya aina mbalimbali. Vyakula vya nafaka ambayo haijakobolewa kama vile mkate, nafaka yenyewe mfano dona, tambi au mchele vina virutubisho na nyuzinyuzi kuliko vyakula vinavyotokana na nafaka zilizokobolewa.
Fanya mazoezi ya Viungo vya Mwili
Unahitaji kufanya mazoezi bila kujali umri wako ili kuwa na afya njema. Ni vizuri kuwasiliana na daktari au mtaalamu wa mazoezi kabla ya kuanza kufanya mazoezi yoyote mapya, kwa maana mazoezi yanayofaa yanategemeana na umri na afya ya mtu. Pumzika au pata muda wa kutosha kulala usingizi
Mabadiliko ya maisha yameongeza vikengeushafikira na hekaheka za maisha ya sasa na kufanya watu wasiwe na wakati wa kutosha kulala. Kulala na kusinzia vya kutosha muhimu kwa ajili ya ukuzi na maendeleo ya watoto na vijana, kujifunza na kukumbuka habari mpya, kudumisha usawaziko unaofaa wa homoni zinazosaidia kumeng'enya chakula na uzito wa mwili, kudumisha moyo wenye afya nzuri na kuzuia magonjwa.
Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook
DOWNLOAD APPLICATION HAPA..!!
LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOK
Post a Comment