Breaking news

WATU 11 WANASADIKIKA KUPOTEZA MAISHA MWANZA

Watu 11 wanasadikika kupoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea leo saa 11 asubuhi katika eneo la Hungumalwa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza ikihusisha daladala na basi la Super Shem lililokuwa likitokea Mbeya kuja Mwanza.

Majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa kwenye basi wamesema basi lao lilikuwa kwenye mwendo mkali na lilipofika eneo la tukio ghafla daladala hiyo iliingia barabarani na hivyo dereva wa basi kushindwa kuikwepa.

Waliopoteza maisha na kujeruhiwa ni abiria waliokuwa kwenye daladala
Post a Comment

Post a Comment