Bunge limeiagiza Serikali kuhakikisha inaleta majibu ya kuridhisha bungeni kuhusu hatua zilizochukuliwa kufuatia tetemeko là ardhi mkoani Kagera.
Naibu Spika Dk Tulia Ackson ameiagiza Serikali kuhakikisha inatoa majibu hayo baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, George Simbachawene kutoa kauli ya Serikali bungeni leo.
Waziri huyo amesema Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Jenista Mhagama wapo eneo là tukio kuendelea na tathimini.
Kwa mujibu wa Simbachawene, mpaka asubuhi hii idadi ya vifo ni 17 majeruhi waliopo hospitali ni 169 walioruhusiwa ni 83 hivyo kufanya jumla ya majeruhi kuwa 252.
Amesema nyumba za makazi zenye nyufa ni 1264 majengo ya taasisi yaliyoripotiwa kuanguka ni 44.
Tangaza hapa charzdangote@gmail.com
Post a Comment