Almaz Ayana ameshindia Afrika dhahabu ya kwanza Rio na kuvunja rekodi ya dunia
Almaz Ayana ameishindia Afrika dhahabu ya kwanza katika michezo ya Olimpiki mjini Rio na kuvunja rekodi ya dunia mbio za mita 10000 wanawake.
Ayana aliwaacha nyuma wapinzani wake mbio zikiwa katikati na kuendelea hadi mwisho, muda wake ukiwa dakika 29 sekunde 17.45.
Rekodi ya awali iliwa 29:31.78 na iliwekwa na Mchina Wang Junxia mwaka 1993. Mkenya Vivian Cheruiyot ameshinda fedha naye raia mwingine wa Ethiopia Tirunesh Dibaba akachukua shaba.
Post a Comment