today news

Muhongo ataka mchakato wa kufungua biashara uwe mwepesi

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amefunga maonyesho ya biashara ya kimataifa huku akisisitiza kasi ya kufungua biashara na mikataba kwa wawekezaji.

Amesema ni Tanzania pekee ndiyo nchi ambayo ili kuanzisha biashara inabidi ufuate hatua tisa.

Amesema ili kuendana na kasi ya dunia na kukimbizana na harakati za kukua kiuchumi inabidi siku za kuanzisha biashara zipungue na kubaki tatu.

"Naomba mwaka ujao mniite kufunga maonyesho tena ili niangalie kama Wizara ya Viwanda, biashara na Uwekezaji mmelifanyia Kazi hili" amesema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo amesema hatua ambazo mtu anachukua kuanzia kufuatilia vibali, leseni hadi kuanza biashara zipo 21 na kutaka zipungue na zibaki tano.

" Hatuwezi kwenda hivi zibaki tano , mtu akianza kufuatilia leseni Jumatatu hadi ijumaa awe amepata , tutumie kompyuta tuachane na kukusanya makaratasi, mafaili inawezekana ndiyo inachangia kuchelewa" amesema.

Wakati huo huo rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alisisitiza kuwa wafanyabiashara wadogo watafutiwe masoko ili kuwainua kiuchumi.

na biashara zao zinavutia hivyo watafutiwe masoko ya uhakika ili wasonge mbele"amesema Kikwete.

Jiunge na BONGOHOTZ.COM sasa

Usipitwe!! kupitia FACEBOOKTWITTER naINSTAGRAM kupata habari ndani ya sekunde kila inapotufikia..!! Usiache ku download application play store BOFYA HAPA KU DOWNLOAD....... LIKE PAGE YA BONGOHOTZ KWENYE FACEBOOKLIKE PAGE 

DOWNLOAD APP YA "BONGOHOTZ" UPATE NOTIFICATION KWA KILA KITU KIPYA 

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI

Post a Comment

Post a Comment