Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameendelea kusisitiza kuwa suala la kuzuiwa kurushwa moja kwa moja kwa matangazo ya Bunge si lake bali lilipitishwa na wabunge wenyewe. Nape amesema hayo alipozungumza mjini Dodoma hivi karibuni.
Amesema yeye ni msimamizi wa Serikali, watu waache kupotosha, alichokifanya ni kulinusuru Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kwa miaka 10 mfululizo ambayo Bunge lilishindwa kuwalipa fedha zao ambazo ni Sh4.5 bilioni za matangazo ya kila mwaka.
Hata hivyo, amesema suala hilo liwe fundisho kwa wabunge, kwani kuna vitu huvipitisha bungeni baada ya muda wanaona madhara yake nakuanza kulalamika.
Post a Comment