Rais magufuli akiwa na marais wastaafu
Rais John Magufuli ameendelea
kutofautiana kimkakati na watangulizi wake, akisema hakuna mtu atakayeshikilia vyeo viwili kwa wakati mmoja baada ya kumteua kimakosa mbunge kuwa mkuu wa wilaya.
Mfumo huo wa Rais Magufuli unakwenda tofauti na watangulizi wake, Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa ambao waliteua wabunge kuwa wakuu wa mikoa na wilaya.
Dk Magufuli alibainisha hilo jana wakati akitoa ufafanuzi uamuzi wake wa kutengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Fatma Hassan Toufiq.
“Mtu mmoja kazi moja,” alisema Rais Magufuli baada ya kufafanua kuwa kuna makosa yalifanywa wakati wa uteuzi huo.
Post a Comment