today news

Majangiri Wamnyima Usingizi Maghembe



Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe


Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema Serikali haiwezi kukubali kupoteza rasilimali za Taifa kwa watu wachache.

Akizungumza juzi kwenye futari iliyoandaliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Christopher Gachuma, Profesa Maghembe alisema Serikali imedhamiria kukomesha ujangili.

Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha inadhibiti ujangili kila kona kwa sababu hatuwezi kukubali kupoteza kipato cha Taifa hivihivi, kwa hiyo niwaombe nyinyi wananchi toeni taarifa na ushirikiano kwa Polisi,” alisema.

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza, Salum Bara aliwataka Waislam kudumisha amani na kufanya mambo mema

Post a Comment

Post a Comment