Mwanza. Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali ombi la Chadema la kuruhusiwa kufungua kesi dhidi ya amri ya Jeshi la Polisi la kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa kutokana na maombi hayo kutokidhi matakwa ya kisheria.
Uamuzi huo umetolea muda mfupi uliopita na Jaji Mohamed Gwae baada ya kukubaliana na pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi, Robert Kidando na Obadia Kajungu waliodai waleta maombi hawakutumia kanuni sahihi kuwasilisha ombi hilo.
Katika uamuzi wake, Jaji Gwae amesema waleta maombi walijielekeza vibaya kisheria kwa kutonukuu kwa usahihi baadhi ya vifungu muhimu vinavyoipa Mahakama mamlaka na haki ya kusikiliza na kuamua maombi yao ambapo aliwaelekeza kukata rufaa iwapo hawajaridhika au wapeleke maombi mapya.
Post a Comment