Mlemavu wa viungo amegongwa na basi la mwendokasi na kufa papo hapo usiku huu, eneo la Kariakoo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Lucas Mkondya amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 2.00 usiku makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru na kwamba, mwili wa mlemavu huyo wa kiume umeokotwa vipandevipande.
Nkondya amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva, kwani tukio hilo limetokea karibu na makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru ambako kuna mataa, hivyo alitegemea basi lingekuwa kwenye mwendo wa kawaida.
Post a Comment