Waziri Mkuu kassim Majaliwa, amemjibu kiongozi wa upinzani Bungeni Freeman Mbowe, aliyehoji siku za hivi karibuni kitendo cha Serikali kutotoa hati maalumu ya mwongozo (Instrument) inayoitambulisha serikali iliyopo madarakani kwa mujibu wa sheria.
"Instrument ipo, na tayari imeshasainiwa na rais kwa mujibu wa sheria, kwa sasa mchakato wa kuitangaza kwenye magazeti ya Serikali inaendelea, amesema Waziri Mkuui Majaliwa
Amesema viongozi wote wa serikali wapo kwa mujibu wa sheria na kanuni za serikali.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema haya wakati alipokuwa akihitimisha hotuba yake ya kulitaka bunge likubali kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi yake kwa mwaka wa fefdha 2016/17
Post a Comment