latest news

MAWAZIRI WALIOSHINDA KUWASILISHA FOMU ZA MAADILI WATOA SABABU HIZI KWA RAIS MAGUFULI




Mawaziri watano waliopewa mpaka jana saa 12 jioni kurudisha fomu za maadili, watoa sababu zilizowafanya washindwe kurudisha kwa wakati. 

Makamba: Anasema huwa anamtumia mwanasheria wake kuzipeleka fomu zake kila anapojaza lakini kwa wakati huu mwanasheria wake alikuwa na udhuru wa muda mrefu na aliyemtuma hakufanya hivyo.

Dr Mahiga: Anasema yeye alibanwa na majukumu hasa safari za nje hivyo kushindwa kupata muda wa kuzipeleka fomu hizo tume, japo amekiri kuwa agizo la Rais limetoa somo zuri kuhakikisha kila jambo linafanyika kwa wakati.

Kitwanga: 
Yeye anasema fomu zake alizipeleka toka tarehe 4 Januari na ameshangaa kwamba anatajwa japo jana baada ya tume ya maadili kuzitafuta zilipatikana.

Mpina: Yeye anasema alishindwa kupeleka fomu kutokana na kutojua mshahara wake.
Jana hiyohiyo alimwita mhasibu na kujua mshahara wake na fomu akazirudisha.

Prof. Ndalichako sababu zake hazijapatikana japo naye jana hiyohiyo alituma mwakilishi kuzirudisha fomu zote tume ya maadili.


Post a Comment

2 Comments

  1. Anonymous4:42 PM

    kweli wamezidi uongo sasa

    ReplyDelete
  2. Anonymous4:43 PM

    itabidi wachukuliwe hatua kali

    ReplyDelete