WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO NCHINI ASA WAJA NA MWAROBAINI YA KUONDOA TATIZO LA UHABA WA MAFUTA NCHINI - Swahili Viuhapa
MKUU
wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu kushoto akipokea mmoja ya
miche ya michikichi 30,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao
Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin
Ringo kwa ajili ya kuwakabidhiwa DAWASA kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha
Mazingira (Dawasa) Mhandisi Modester Mushi ,kwa ajili ya kuhifadhi
mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi kipato
MKUU
wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu katika akimkabidhi miche ya
michikichi 30,000 Mkuu wa Kitengo cha Mazingira (Dawasa) Mhandisi
Modester Mushi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu
na kuwaongezea wananchi kipato ambapo miche hiyo ilitolewa na Wakala
wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA)kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa
Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt
Justin Ringo
MKUU
wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu katika akimkabidhi miche ya
michikichi 30,000 Mkuu wa Kitengo cha Mazingira (Dawasa) Mhandisi
Modester Mushi kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu
na kuwaongezea wananchi kipato ambapo miche hiyo ilitolewa na Wakala
wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA)kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa
Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt
Justin Ringo
MKUU
wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati wa halfa
hiyo kulia Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo
nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo
Mkuu
wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akisistiza jambo wakati wa
halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za
Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo
Mkurugenzi
wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini (ASA) Makao
Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo akizungumza wakati wa halfa hiyo
kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu
Mkuu
wa Kitengo cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam
(Dawasa) Mhandisi Modester Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo
Wakiangalia Bwawa
Sehemu ya mbegu za mchikichi zilizopo kwenye Shamba la Mbegu la Mwele
NA OSCAR ASSENGA,MKINGA.
WAKALA
wa Mbegu za Kilimo Tanzania (ASA) umesema kwamba lengo lao kubwa hivi
sasa ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa mafuta linapungua nchini kwa
kutumia zao la mchikichi ambalo ni zao la kimkakati kwa kuzalisha
mafuta.
Hatua hiyo inatajwa kwamba itapunguza gharama kubwa
ambazo Taifa linaingia kuagiza mafuta kutoka nje na hivyo kuondokana na
adha ya kutumia fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya bidhaa hiyo.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mazao Wakala wa Mbegu za
Kilimo nchini (ASA) Makao Makuu Morogoro Dkt Justin Ringo wakati wa
halfa ya makabidhiano ya Mbegu za Michikichi 30,000 kwa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Dar es Salaam (Dawasa)kwa ajili ya
kuhifadhi mazingira kando kando ya Mto Ruvu na kuwaongezea wananchi
kipato
Halfa hiyo ilifanyika kwenye Shamba la Mwele lililopo
kata ya Maramba wilayani Mkinga ambalo limepewa jukumu la kuzalisha
mbegu za michikichi, Miche hiyo ilitolewa na Wakala wa Mbegu za Kilimo
nchini (ASA)
Alisema mbali na michikichi na wameongeza maeneo ya
mengine makubwa ya hekta kwa ajili ya kuzalisha zao la alizeti na
mashamba mengine waliopanga kuzalisha mazao mengine kwa kuona shida
iliyojitokeza wakaona wazalishe mazao ya alizeti.
“Lengo kubwa
ni kwenda sambamba na msisitizo wa seriali kuhakikisha mafuta
yanapatikana nchini kwa kupatikana mbegu bora za alizeti na michikichi
lakini nipende kuwakaribisha wananchi wajipatie mbegu bora za mazao
kuinua nchi kiuchumi wao”Alisema
Alisema michikichi hiyo
inatokana na Wakala huo kukuza miche kwa kushirikiana na Taasisi ya
Utafiti Tanzania (TARI) wanapata miche kutoka kwao wanaikuza na kuitoa
kwa wadau mbalimbali kama walivyofanya kwa Dawasa.
Awali
akizungumza wakati akipokea mbegu hizo za Michikichi, Mkuu wa Kitengo
cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa)
Mhandisi Modester Mushi alisema pamoja na wao kutoa huduma ya maji safi
na usafi wa mazingira wanatumia maji kutoka kwenye vyanzo vya mito na
hapo lengo lao linaanzia kwenye mto Ruvu ambao unawapatia maji zaidi ya
asilimia 92 huduma inayotolewa Dar Es Salaam na Pwani.
Alisema
kwamba wameamua kuchukua miche hiyo ya michikichi pamoja na uelekeo wa
Serikali katika kuona kwamba wanataka kuzalisha mafuta nchini wao
wameona ni zao ambalo litasaidia kutunza chanzo.
Aidha alisema
kingo za Mito kwa hivi sasa zinaathirika kwa shughuli za binadamu
ikiwemo kilimo, ufugaji hivyo shughuli hizo wananchi wanafanya ili
waweze kupata mahitaji yao mbalimbali.
“Hivyo ni tuna imani
kwamba upandaji zao la michikichi mwananchi badala ya kupanda mazao ya
muda mfupi kupitia michikichi ataweza kuvuna mara nne kwa mwaka na
atakuwa mmojawapo anachangia hatua na jitihada za serikali katika
kutengeneza mafuta na kipato chake kitabadilika na kitakuwa zaidi ya
hivi sasa”Alisema
Alisema miche hiyo itakapokuwa pembezoni ya
mto itasaidia kupunguza shughuli za mara kwa mara zinazohusisha kugusa
ardhi kulima na itapunguza kiasi kikubwa tope au mchanga ambao unatokana
na shughuli hizo unaopelekea mamlaka kuwa na gharama za juu kwenye
uzalishaji wa maji.
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya
Mkinga Mkoani Tanga Kanali Maulid Surumbu alisema mara kwa mara Waziri
Mkuu Kasim Majaliwa amekuwa akielekea Kigoma kuhamasisha zao la
michikichi ili liweze kuzalishwa kwa wingi ili mwisho wa siku waweze
kuondokana na tatizo la mafuta nchini.
Mkuu huyo wa wilaya
aliwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mkinga zao hilo la mchikichi hata
wilaya hiyo linastawi vizuri hivyo watumie fursa ya uwepo wa shamba la
mwele ambalo limepewa jukumu lakuzalisha zao la michikichi kutoa mbegu
kwa wananchi.
Hata hivyo alisema wilaya hiyo wana mashamba mengi
yanayomilikiwa na Taasisi, Halmashauri na watu binafsi ambapo mashamba
hayo yakitumika vizuri kuzalisha zao la mchikichi nao watakuwa miongoni
mwa dau watakaochangia kupunguza gharama zinazoingiwa na serikali
kuagiza mafuta nje ya nchi.
Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb
The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.
https://www.swahili.viuhapa.com/wakala-wa-mbegu-za-kilimo-nchini-asa-waja-na-mwarobaini-ya-kuondoa-tatizo-la-uhaba-wa-mafuta-nchini-swahili-viuhapa/
Post a Comment