Bank

Tanzania Commercial Bank yaombwa kupanua wigo wa huduma zake nchini - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Fatuma Almasi Nyangassa, ameiomba benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) kupanua wigo wa huduma zake katika wilaya hiyo ili kuwawezesha wajasiliamali kufikiwa huduma za kibenki na hivyo kupata fursa ya kujikwamua kiuchumi.

Nyangassa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa tawi jipya na la kisasa la benki hiyo , lililopo karibu na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni, ambalo ni sehemu ya mkakati wa kutimiza azma ya kitaifa ya kufikisha huduma za kifedha kwa kila mtanzania.

Amesema katika wilaya ya Kigamboni kuna wafanyabiashara na wajasiriamali wengi ambao wanahitaji huduma za kifedha, na akatumia fursa hiyo kuiomba benki ya TCB kuzidi kongeza na kuboresha miundombinu ya huduma zake ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

“ Wilaya yetu ya Kigamboni inazo shughuli nyingi za kiuchumi vikiwemo viwanda mbalimbali, vikubwa na vidogo, hivyo ujio wa benki hii ya TCB utarahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki na hivyo kuiunua ufanisi na ukuaji wa shughuli za uchumi,” alisema Fatma Nyangassa.

Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, alisema benki hiyo kwa sasa ni miongoni mwa benki kumi bora katika utoaji huduma hapa nchini, na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi katika tawi hilo kujipatia huduma mbali mbali, ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.

Alisema Moshingi; “ Benki ya TCB pia inajali jamii hasa katika sekta za afya na elimu, na imewekeza katika kuhakikisha kuwa inaunga mkono program mbalimbali za sekta hizo muhimu ili kufanikisha azama ya serikali ya Awamu ya Sita kuinua kiwango cha maisha cha watanzania.

Moshingi amesema kuwa tawi la Kigamboni ni tawi la kwanza kwa wilaya hiyo, na kuongeza kuwa benki hiyo ina mtandao mpana nchini, ikiwa na inatoa huduma kupitia matawi mengine 82, na kuahidi kuwa TCB itaendelea kupanua wigo wa huduma zake ili kila mtanzania na mteja wa benki hiyo afikiwe na huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa.

:Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa (kushoto), akifungua pazia la jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya  la Benki ya Tanzania Commercial Banki Kigamboni Hafla hiyo imefanyika  leo katika ofisi za tawi hilo kigamboni jijini Dar es Salaam kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, Tawi la Tanzania Commercial Bank limekuwa ni tawi la kwanza katika Wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa (watatukulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi  wa tawi la Tanzania Commercial Bank Kigamboni. Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za tawi hilo lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, kulia ni Meneja wa Tawi la hilo Lameck Bubewa.

Meneja wa Tawi  wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Lameck Bubewa akizungumza wakati wa hafla wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo lililofunguliwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa (katikati),akizungumza wakati wa hafla wa uzinduzi wa tawi la benki ya Tanzania Commercial Bank  lililofunguliwa katika wilaya hiyo  kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, pamoja na Mkurugenzi Tehama na Uwendeshaji wa Tanzania Commercial Bank Jema Msuya








viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/tanzania-commercial-bank-yaombwa-kupanua-wigo-wa-huduma-zake-nchini-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment