habari

TAFAKURI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA KATIKA MUKTADHA WA ‘MAHAKAMA MTANDAO’ - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye ni mgeni
mwalikwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria mkoa wa Singida mwaka
2022, Dk. Binilith Mahenge akizungumza.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Singida Alu Nzowa akizungumza kwenye maadhimisho hayo

Mwakilishi wa Mawakili wote wa Mkoa wa
Singida Wakili Peter Ndimbo

akizungumza.

 Mkuu wa Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Singida,
Salige akizungumza

  Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida
wakishiriki kikamilifu maadhimisho hayo.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa dini wakiwa
kwenye maadhimisho hayo.

Mahakimu na Mawakili wa Mahakama za Singida.

 Mahakimu na Mawakili wa Mahakama za Singida.

Baadhi ya Watendaji wa Mahakama mkoani hapa.

Watendaji wa Mahakama Mkoa wa SingidKundi la baadhi ya watumishi wa mahakama.

Baadhi ya wawakilishi wa Taasisi mbalimbali
za serikali wakishiriki kikamilifu maadhimisho hayo.

Picha ya pamoja.

Baadhi ya wanafunzi

Vikundi vya ngoma na Burudani. 

 Kundi la picha ya baadhi ya wananchi
waliohudhuria sherehe hizo.

Na
Godwin Myovela, Singida

TANGU
mwaka 1996, Mahakama ya Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya sheria nchini kwa
lengo la kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za mahakama kwa mwaka husika.
Maadhimisho haya kila mwaka hufanyika kwa kuongozwa na tafakuri mahsusi
inayojadiliwa kama dira ya utendaji kazi wa mahakama.

Nichukue
nafasi hii kupongeza hatua hiyo ambayo dhahiri inalenga kuwakutanisha wadau wa
mahakama na wananchi katika dhana pana ya kupeana elimu sambamba na
kukumbushana mambo kadha wa kadha ili kwa pamoja na umoja kuweza kutekeleza
majukumu ya utoaji haki kwa mujibu wa 
viapo.

Pia
kwa kutambua umuhimu wa kuifanya mahakama kufikiwa na wananchi ambao ndio
walengwa wa huduma za mahakama; tangu mwaka 2017, maadhimisho haya yamekuwa
yakiongezwa msisitizo kuhakikisha chombo hiki kinazingatia pamoja na mambo
mengine, mambo ya ushirikishwaji wa wadau, utawala bora, uwajibikaji na
matumizi bora ya rasilimali, upatikanaji wa haki kwa wakati ili kujenga imani
ya wananchi.

Binafsi
nitajikita kwenye eneo moja la Mahakama Mtandao katika dhima ya kauli mbiu ya
mwaka huu isemayo; “Zama za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda: Safari ya Maboresho
kuelekea Mahakama Mtandao”

 

Kupitia
maadhimisho ya mwaka huu tumeelezwa kwamba Mahakama Mtandao (e-judiciary) ni
Mahakama inayoendesha shughuli zake zote za utoaji haki na zile za kiutawala
kwa njia ya kielektroniki au kwa lugha nyepesi kwa kutumia TEHAMA (emails, simu
za mkononi, internet na mitandao mbalimbali ya kijamii) kikamilifu katika
shughuli zake zote.

Kwa mujibu
wa mahakama huduma hiyo mpaka sasa inaendelea kufanyika kuanzia eneo la ufunguaji
wa mashauri, usikilizwaji, uhifadhi wa nyaraka, utunzaji wa taarifa za kiutumishi,
udhibiti wa rasilimali na mifumo ya malalamiko

Pia kuna maeneo mengi ambayo
Mahakama imeyaboresha au kuyaanzisha yanayoonesha dhahiri kuwa chombo hiki kinasafiri
kuelekea Mahakama Mtandao, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu, uanzishaji wa
vituo jumuishi vya utoaji haki, uanzishaji wa mahakama inayotembea na matumizi
na maboresho ya Tehama.

 Hata hivyo, tumeelezwa kwamba, kwa sasa kuna faida nyingi ambazo watumiaji wa huduma za kimahakama wameanza
kuzipata kutokana na uwepo wa mahakama mtandao ikiwemo; urahisi na uharaka
usikilizwaji wa mashauri kuanzia kwenye uwasilishwaji wa mashauri mahakamani,
usajili wa mashauri lakini pia upatikanaji wa nyaraka na taarifa za mashauri.

Wadaawa wanaweza kuwasilisha shauri bila kufika mahakamani shauri
likapokelewa, likafunguliwa na mhusika akapewa mrejesho huko huko alipo. Pia
shauri linaweza kuendeshwa kwa kutumia mfumo wa video. Lakini pia mahakama
mtandao inapunguza gharama za uendeshaji wa mashauri kwa wadaawa, wadau na mahakama
yenyewe.

Imethibitika kwa kutumia mahakama mtandao gharama za uendeshaji wa
mashauri zimeendelea kupungua kwa kiasi kikubwa kwa pande zote katika shauri,
na hususani kwenye nyanja ya mahakama inayotembea mpaka sasa takribani mashauri
1,208 yamesikilizwa na watu wapatao 13,668 na huduma hii.

Aidha, mahakama mtandao inaongeza uwazi katika shughuli za
kimahakama. Wadaawa wanaweza kufuatilia mwenendo wa shauri kupitia mtandao bila
kukutana na urasimu wa aina yoyote.

Pia mahakama mtandao inasaidia taasisi kupata takwimu sahihi za
mashauri na kwa wakati. Inaongeza ufanisi katika kutekeleza jukumu la msingi la
utoaji haki, na kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Zaidi, ni chombo cha kukusanyia mapato ya serikali ambayo hapo
awali kulikuwa na upotevu mkubwa. Lakini pia taasisi inaitumia mahakama mtandao
kama chombo cha kufanyia tathmini ya mtu mmoja mmoja au mahakama husika na
mahakama kama taasisi kwa ujumla.

Changamoto za Mahakama Mtandao

Suala la elimu kuhusu matumizi ya
huduma hiyo bado ni changamoto ikizingatiwa wananchi wengi wanashindwa kuendana
na maboresho ya huduma hiyo ya kitehama kutokana na sababu za kimazingira kwa
wengi hasa vijijni kukosa mawasiliano ya kimtandao huku wengine wakikosa elimu
ya namna ya kutumia huduma hiyo.

Ni dhahiri, mpaka sasa kuna ombwe
kubwa la wengi kupata usumbufu mkubwa hasa kwenye eneo la kusajili kesi au
kufuatilia tarehe za kesi zao kutokana na kukosa simu za viganjani na vifaa
vingine vinavyoendana na huduma hiyo, huku hata wengine wenye vifaa hivyo nao
wakijikuta wanakosa wataalamu stahiki wa kuwaelekeza nini cha kufanya kutokana
na uchache wa wataalamu wa sekta hiyo ndani ya mahakama.

Mathalani sio mahakama zote zenye
TVs na vifaa vya kutosha kuweza kuendesha kesi kwa video conference hali
inayopelekea changamoto ya hata namna ya kuthibitisha vielelezo vinavyotolewa
kupitia huduma hiyo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa
na chama cha mawakili nchini (TLS) kwenye eneo hilo kupitia kilele cha maadhimisho
ya siku ya sheria mwaka huu-mkoani hapa-imebainika, pamoja na mambo mengine,
pia hata usajili wa kesi kwa njia ya mtandao bado kuna urasimu; imeelezwa hata
ukisajili kwa njia hiyo bado tena utatakiwa kupeleka tena nyaraka halisi
mahakamani hali inayoleta mkanganyiko kwa wananchi.

Pia upatikanaji wa mtandao kwa
maeneo mengi ni changamoto huku pia wadau wengine kama mabaraza ya ardhi na
tume za ajira za usuluhishi na maamuzi hawajaungwa hivyo kufifisha huduma hiyo
muhimu, na chombo hicho kujikuta kikitengeneza double standard kwenye utoaji haki nchini.

Binafsi naamini na naunga mkono
ushauri uliotolewa na TLS kuwa mfumo huu wa mahakama mtandao kwanza; uingizwe
kwenye mtaala wa mafunzo ya wanasheria vyuoni ili iwe sehemu ya ujuzi wanaopata
kabla ya kuingia kazini.

Pia, kuwe na elimu endelevu kwa
mawakili waliopo kazini na wadau wengine wote wa mahakama na wananchi ili elimu
hiyo anuai ieleweke ipasavyo na kwa kiwango cha kutosha kwa kila mtu kuweza
kunufaika nayo.

Katika kufanikisha hilo, mahakama
haina budi kuajiri wataalamu wa kutosha wa taaluma ya Habari na Mawasiliano
walau kila ilipo mahakama ya wilaya ili kuwezesha watumiaji wa huduma hiyo kuwa
na ufanisi katika matumizi yake.

Lakini kupitia maadhimisho hayo
ilishauriwa mahakama ifanye kazi kwa ukaribu na makampuni wamiliki wa mitandao
kama TTCL, Vodacom, Tigo, Halotel, Zantel kwa pamoja kufanikisha maboresho ya
matumizi ya huduma hiyo ya mahakama mtandao hasa kwa maeneo ya vijijini.

Na kama maoni hayo muhimu ya wadau
yatazingatiwa; basi; dhima hiyo huenda sasa ikawa ndio mwongozo sahihi kwa Mahakama
ya Tanzania katika muktadha chanya wa Mahakama Mtandao yenye tija kwa wananchi
kuona, kupata taarifa, maelekezo na huduma zote muhimu bila hata kufika moja
kwa moja kwenye majengo ya mahakama.








viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/tafakuri-ya-maadhimisho-ya-siku-ya-sheria-katika-muktadha-wa-mahakama-mtandao-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment