habari

TAA yatoa Msaada samani katika Shule ya Msingi Kinyerezi Jica - Swahili Viuhapa

featured image


viuhapa

Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) leo
imekabidhi msaada wa samani ya Meza kumi (10) na Viti kumi (10) kwa
ajili ya matumizi ya Walimu katika shule ya msingi Kinyerezi Jica
iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Sera ya TAA ya kurudisha kwa Jamii (Corporate Social
Responsibility).

 

Akikabidhi Samani hizo Mwenyekiti
wa kamati ya kurudisha kwa jamii (CSR) Bw, Maxmilian Mahangila kwa niaba
ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA amesema, dhumuni la msaada huu ni Kuwawezesha
waalimu kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi ili waweze kufundisha
wanafunzi kwa viwango vya ubora Zaidi, lakini pia kujenga mahusiano
mema kwa jamii nzima.

 

 ‘’ Hawa wanafunzi
mnaowafundisha hapa tunawategema sana kuwa viongozi na wafanyakazi wa
baadae serikalini na katika sekta binafsi, hivyo kutoa msaada huu leo ni
kuwawezesha walimu muwafundishe vyema ili waje wasaidie Taifa letu,
kwani Samani hizi tunazotoa zinawasaidia katika kazi zenu mbalimbali za
kuandaa masomo ya kufundisha, kusahisha kazi za wanafunzi na kazi
nyingine nyingi ambazo waalimu mnakuwa nazo’’, alisema Bw, Mahangila.

 

Naye
Mkuu wa shule,Bw. Baraka Baltazar ameishukuru Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege (TAA) kwa kusaidia Samani ambazo ilikuwa ni hitaji la muda mrefu
na muhimu kwa Waalimu wa shule kupata Meza na Viti ili visaidie katika
Matumizi ya shule na kupunguza changamoto katika mazingira ya
ufundishaji.

 

‘‘Tunashukuru sana kwa msaada mkubwa
mliotupatia umesaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa meza na viti
kwa waalimu hivyo ufanisi wa utendaji kazi katika mazingira bora
utaongezeka’’ alisema Mkuu wa shule.

 

Aidha Bw
Baltazar ameainisha changamoto kadhaa ambazo bado zinaikabili shule yake
ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji kutokana na miundombinu kutokuwa
Rafiki hivyo kuitaji kisima pamoja na matanki mawili ya kuhifadhia maji
ya lita 5000, Maktaba kwa ajili ya waalimu na wanafunzi kujiongezea
maarifa pamoja na vifaa vya Tehama kutokana maendeleo ya teknolojia kwa
hivi sasa.

 

Shule ya msingi Kinyerezi Jica
ilianzishwa Januari 2016 baada ya kugawanywa kutoka shule ya msingi
Kinyerezi kutokana na wingi wa wanafunzi waliokuwepo. Shule hii inakua
kwa kasi ambapo kwa sasa inajumla ya madarasa 18 na idadi ya wanafunzi
imefikia wanafunzi 1538 na walimu 51 ukilinganisha na hali iliyokuwepo
wakati shule inaanzishwa ikiwa na madara 6, wanafunzi 587 na waalimu 13.

 

Shule
ya msingi Kinyerezi Jica ni moja ya shule inayofanya vizuri kitaaluma
mwaka hadi mwaka katika kata ya kinyerezi, Halmashauri ya jiji la Dar es
saalam.

Wakati huohuo Katika kutambua mchango
uliotolewa na TAA uongozi wa shule ya msingi Kinyerezi Jica umeipatia
TAA cheti cha kutambua mchango uliotolewa ‘’ Certificate of
Appreciation’’ na kuiomba TAA kuwa Mlezi wa shule ya msingi Kinyerezi
Jica.

Mwenyekiti
wa Kamati ya TAA ya  kurudisha kwa jamii (CSR) kutoka Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege Tanzania  (TAA) Bw. Maxmilian Mahangila katikati akikata
utepe kuashiria  makabidhiano ya msaada wa samani za meza 10 na viti 10
kwa ajili ya matumizi ya  ofisi ya waalimu katika shule ya Msingi
Kinyerezi Jica uliotolewa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
mapema leo.

Afisa
Elimu kata ya Kinyerezi Bi, Radhia Mfalingundi akimkabidhi Cheti cha
kutambua Mchango wa msaada kutoka  TAA (Certificate of Appreciation) Bw.
Maxmilian Mahangila, kwa niaba ya shule ya Msingi Kinyerezi Jica mara 
baada ya kutoa Msaada wa samani  katika shule hiyo.

Picha
ya pamoja kati ya Uongozi na waalimu wa shule ya Msingi Kinyerezi Jica
pamoja na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania mara
baada ya kukabidhi msaada wa Samani za Meza na viti kwa shule hiyo.




viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/taa-yatoa-msaada-samani-katika-shule-ya-msingi-kinyerezi-jica-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment