Burudani

Sita wakamatwa mauaji ya watu wanne Njombe - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

Jeshi la Polisi mkoani Njombe linamshikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne katika matukio matatu tofauti yaliyotokea katika mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Februari 4, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe (RPC), Hamisi Issah amesema mauaji hayo yemetokea ndani ya mwezi Januari mwaka huu.

Kamanda Issah amesema katika tuykio la kwanza Jeshi hilo linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kilimahema kilichopo wilayani Wanging’ombe, Israel Msigwa (39) kwa tuhuma za mauaji ya mwanawe Haskad Msigwa (7) baada ya kumuchapa kwa kutumia nyaya za umeme na fimbo.

Amesema mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo alitoweka na baadaye alikamatwa eneo la Kilosa lililopo mjini Mafinga mkoani Iringa.

“Huu ni ukatili kwani huwezi kutoa adhabu ambayo inaweza kusababisha kifo kwa mtoto” amesema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema Jeshi hilo pia linamshikilia Ambwene Sanga (34) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa chekechea katika shule ya Imalilo iliyopo wilayani Wanging’ombe, Media Kaduma (5).

Kamanda Issah amesema “Mtoto huyo tulimuokota na baba wa kambo wa mtoto huyo alikuwepo wakati wa kumsaka mtoto lakini ndiye aliyehusika na mauaji hayo”.

Pia, Kamanda Issah amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia mkazi wa Sovi mjini Makambako, Joseph Mgunda (35) kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili ambao ni Suzan Mtitu na Kassim Kitamkanga.

Amesema Mgunda ambaye anadaiwa kuwa mganga wa kienyeji aliwaambia marehemu hao kuwa wakipeleka fedha zao kwake anaweza kuziombea na zikaongezeka.

“Mganga huyo aliwaambia ndugu zake ndipo aliposhauriwa kuwa ukitaka usipate shida ni kuwapoteza hawa yaani kuwaua” amesema Issah.

Amesema mpaka sasa watuhumiwa wengine watatu wanashikiliwa kutokana na mauaji ya watu hao wawili.

Amesema Jeshi hilo linaendelea na upelelezi na likikamilisha litawafikisha watuhumiwa hao mahakamani.

logoblog






viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/sita-wakamatwa-mauaji-ya-watu-wanne-njombe-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment