RAIS SAMIA AWAMWAGA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NNE KWA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UVIKO-19 - Swahili Viuhapa
NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza.
WAKATI taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mwanza,ikichunguza ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo ya Uviko-19 katika Halmashauri ya Buchosa, wilayani Sengerema, Rais Samia Suluhu Hassan,ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Paulo Malala.
Akisalimia wananchi wa Wilaya ya Magu akiwa njiani kuelekea Musoma,Rais Samia,alitangaza kutengua uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za Buchosa, mkoani Mwanza,Iringa,Singida na Mbeya kwa matumizi mbaya ya fedha za Uviko-19 huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita akiwekwa kiporo kutokana na uchunguzi
Habari kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa watu kadhaa katika Halmashauri ya Buchosa,wanashikiliwa na TAKUKURU kwa mahojiano na wakituhumiwa kuhusika kwenye ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa madarasa kwa fedha za Uviko-19.
Akitoa taarifa ya fedha za miradi ya Uviko-19 jana kwa Rais Samia,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel, alisema wanawashikilia watu kadhaa ili kuhakikisha wanarejesha fedha hizo.
Halmashauri ya Buchosa ilipokea Fedha za Maendeleo na Mapambano ya Uviko-19 sh.bilioni 2.5 za ujenzi wa vyumba 142 vya madarasa Serikali kujenga vyumba hivyo.
Hivi karibuni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Frank Mkilanya alisema taasisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu Oktoba hadi Disemba 2021,TAKUKURU ilifanya ukaguzi na ufuatiliaji wa miradi 17 ya maendeleo yenye thamani ya sh.9,845,486,066.85.
Aliitaja miradi hiyo ni ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Mwabilanda wilayani Kwimba wenye thamani ya sh.milioni 333,ujenzi wa kituo cha Afya Bulale katika Wilaya ya Nyamagana Sh. milioni 250 na jengo la wagonjwa wa nje kituo cha Afya Sahwa sh. milioni 50.
Mingine ni ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa Gandhi kwa thamani ya sh.milioni 200,ujenzi wa vyoo kwenye shule za msingi za umma sh.bilioni 3.684, miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara kwa sh.bilioni 3.088 na ujenzi wa madarasa na bweni la watoto wenye mahitaji maalum kwa fedha za Uviko-19 kiasi cha sh.bilioni 2.239.
Mkilanya alisema mbali na ukaguzi na ufuatiliaji huo wa miradi hiyo 17, taasisi hiyo inachunguza ubadhirifu wa fedha za Uviko-19 za ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Buchosa,mara utakapokamilika taarifa itatolewa.
Alitoa wito kuwa wananchi mkoani humu kuwa kila mmoja anawajibika kusimamia miradi ya maendeleo inayotokelezwa kwenye eneo lake,hivyo wanapobaini kasoro au ubovu watoe taarifa TAKUKURU kwa sababu rushwa ina madhara makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutokana na kumgusa mwana kila jamii.
Alisema taasisi hiyo itaendelea kusimamia matumizi sahihi ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na serikali pamoja na wafadhili zikiwemo za mapambano ya Uviko-19.
Aidha Novemba 17,mwaka huu, Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo,akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya Sekondari Kalebezo alisema Mheshimiwa Rais anahangaika kutafuta fedha huku na kule ili kuwasaidia wananchi wake halafu anatokea mtu mwingine kufuja fedha hizo, lazima awajibishwe.Mbunge huyo wa Buchosa,aliwatahadharisha watendaji wa serikali kutothubutu kutafuna fedha za Uviko 19 za ujenzi wa vyumba vya madarasa jimboni humo.
Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili
soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.
Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb
The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.
Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania
Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.
vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.
Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.
https://www.swahili.viuhapa.com/rais-samia-awamwaga-wakurugenzi-wa-halmashauri-nne-kwa-ubadhirifu-wa-fedha-za-uviko-19-swahili-viuhapa/
Post a Comment