Duniani

Msitu 35 Ya Mikoa Ya Morogoro, Lindi Na Iringa Kutambulika Duniani. - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

Misitu 35 ya hifadhi ya vijiji kutoka Wilaya tatu za Mikoa ya Morogoro, Lindi na Iringa imeingia katika kanzidata ya Dunia kuwa kati ya misitu ambayo inatambulika duniani, ambapo hali hiyo imetajwa kuwa na mchango mkubwa kwa jamii zinazozunguka misitu hiyo ikiwemo kuwezeshwa katika utuzaji wa misitu.

Hayo yamelezwa na Meneja Mradi wa kuhifadhi misitu kupitia biashara endelevu kwa mazao ya misitu Bwana Charles Leonad katika ziara ya kamati ya siasa ya wilayani Kilosa mkoani hapa ambapo amesema kutambulika kwa misitu hiyo kutatoa fursa kwa mataifa mbalimbali duniani kuwezesha  shughuli za uhufadhi wa mazingira na utunzaji wa misitu.

Amesema mradi wa kuhifadhi misitu kupitia biashara endelevu kwa mazao ya misitu unatekelezwa na shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) kwa kushirikiana na mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) katika Wilaya saba za mikoa mitatu ya morogoro, Lindi na Iringa.

Wilaya zinazotekeleza mradi huo ni Kilosa, Mvomero, Kilolo, Liwale , Nachingwea, Wilaya ya Morogoro na Ruangwa ambapo kupitia mradi huo wakazi wanaozunguka hifadhi za misitu wananufaika na uvunaji wa mazao ya misitu kama mkaa na mbao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw, Majidi Mwanga amekemea tabia ya viongozi wa vijiji kuingilia majumu ya kamati zilizoundwa kusimamia rasilimali za misitu kwani kufanya hivyo ni kuingilia majukumu ya kamati.

“Kamati ya kijiji ni ya kijiji na kamati ya maliasili ibaki kuwa ya maliasili mkikubali serikali ya kijiji kuingilia katika majukumu yenu mtaharibikiwa.” Alisema mkuu wa Wilaya.

Aidha amewataka wananchi wilayani  kilosa waliobahatika kufikiwa na mradi huo kutumia vizuri maarifa wanayopatiwa na waatalam ili yaweze kuwasaidia baada ya mradi kumalizika.

Nae katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilosa bwana shabani Mdoe ameipokea TFCG pamoja na mjumita kwa kazi kubwa walioifanya katika kutoa elimu juu ya utunzaji wa misitu asili wilayani humo.

Amesema chama kimeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na TFCG kwa kushirikiana na MJUMITA ya kuelimisha wananchi juu ya uhifadhi wa misitu asili kwani awali elimu  juu ya mradi wa MKAA ENDELEVU ilikuwa haitoshi hali iliyofanya watu wengi kuanza kupotosha juu ya mradi huo.

“Na mimi nilikuwa kati ya watu ambao walikuwa hawaelewi kabisa kuhusu mkaa endelevu nilikuwa nikisikia  mkaa endelevu ni shughuli ya kukata miti kutoka hapa mpaka kule tu lakini kupitia ziara hii tumejifunza vitu vingi.” Alisema katibu.

 

logoblog

Thanks for reading Msitu 35 Ya Mikoa Ya Morogoro, Lindi Na Iringa Kutambulika Duniani.






viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/msitu-35-ya-mikoa-ya-morogoro-lindi-na-iringa-kutambulika-duniani-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment