ARDHI

KUKITHIRI KWA MIGOGORO YA ARDHI YATAJWA KUWA CHANZO KIMOJAWAPO CHA MAUAJI -ARUSHA - Swahili Viuhapa





viuhapa

Na.Vero Ignatus,Arusha

 Majaji na Mahakimu
wametakiwa  kuwa na utu katika mashauri
mbalimbali wanayosikiliza na kuyatolea maamuzi, pamoja na kupinga  vitendo vya rushwa ambayo ni adui wa
haki,ambapo wiki hiyo imekwenda  sambamba na mwaka wa kazi  Kimahakama wa mwaka 2022

Hayo yamesemwa na Jaji Mfawidhi kanda ya Arusha Mosses
Mzuna ,Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya sheria  2/2/2022,ambapo aliekemea mambo yanayotokea
mkoani humo  ikiwemo kukithiri kwa mauaji
kwa wanafamilia au jamii, ambayo baadhi hutokana na migogoro ya ardhi,ubomoaji
wa majengo/ nyumba bila amri halali, wakati kuna mashauri yanaendelea  mahakani,pamoja na  kutumia madalali ambao hawajasajiliwa.

Mzuna  alisema kumekuwa na  kitendo cha kuchelewa kwa upelelezi wa
mashauri na  kuchukua muda mrefu, jambo
ambalo husababisha  kudhoofisha kasi ya
usikilizwaji wa mashauri kwa wakati,Ambapo amesema  tatizo hilo lisipotibika hawataweza kutimiza malengo
ya kumaliza mashaurikwa wakati,hivyo amezitaka ofisi zinazohusika lisimamie
jambo hilo

Aidha amesema changamoto ambayo wanakabiliana nayo ni
pamoja na wanafamilia kutokufungua mashauri ya mirathi mahakamani kwa wakati,
hivyo kuchochea migogoro ya kifamilia na hatimaye kupelekea mashauri ya msingi
kuchelewa,pia  jamii kutokutumia njia ya
usuluhishi kama njia mbadala hadi h,upekelea kufikishana mahakamani hata kama
suala ni dogo

‘’Ardhi
isiwe sababu ya kusababisha hadi sisi wana arusha kuuwana jamani ,halafu
mnasubiria siku ya mahakama ndipo mnakwenda kuvunja kweli?msiwasababishe majaji
na mahakimu waonekane hawana maamuzi sahihi, Harutakubali majaji na mahakimu
simameni katika haki wasiwepo watu kukuonyesha wewe kesi ipo mahakamani lakini
anakuja kuvunja simameni kidete katika hili’’Alisisitiza Jaji Mzuna

Kwa upande wake mkuu wa
mkoa John Mongela ameupongeza uongozi wa mahakama ya Arusha kwa kazi
kubwa inayofanyika katika wiki nzima iliyopita, kwa kujihusisha na jamii kwa
kutoa msaada wa kisheria ,kwani kulikuwa na  baadhi ya mambo yalikuwa katika ofisi yake
ambapo baadhi wananchi wametoa shuhuda, kwamba wamefahamu jambo gani wafanye
ili kupata haki zao.

Mongella alisema
kuwa jambo hilo limenawasaidia  mihimili
mingine katika kuhakikisha kunakuwa na utulivu kwa jamii,kwani kazi kubwa
inayofanywna mahakama inachangia kwenye majukumu yao ya kiutendaji,pamoja na
kuhakikisha   usalama na utulivu kuwepo ,hivyo ameahidi kuwa
karibu na mahakama pale wanapohitajika na kuhakikisha kwamba mhimili huo
unakuwa imara zaidi.

Kwa upande wake wakili wa serikali mfawidhi
aliyeiwakilisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Veritas Mlay alisema
katika kuelekea mahakama ya mtandao katika zama za mapinduzi ya nne ya viwanda
inaondoa mipaka kati ya utaratibu ulikuwa umezoeleka kwa muda mrefu wa mtu
kuzoeleka kuwepo mahali Fulani kimwili na kutumia utaratibu wa kidigitali wa
matumizi ya tehama

Amesema kwa upande wa mahakama 2015-2016 iliweka azma Madhubuti
ya kuweka marekebisho makubwa katika mfumo wa matumizi ya tehama kwa ujumla,aidha
hatua ya maboresho kuelekea mahakama ya mtandao ilikolea Zaidi mwaka 2018 ambapo
Jajimkuu wa Tanzania alitoa kanuni ya ufunguaji mashauri kwa njia ya mtandao
kupitia tangazo la serikali no 148 ambazo zimewezesha mashuri kufunguliwa masaa
24.

Amesema mabadilio ya maisha na ufanyaji biashara  na mambo mengine yanayotokea katika Maisha ya
mwanadamu kipekee yanakwenda sambamba na huduma ya utoaji haki,hivyo huduma za
utoaji haki hazina budi kuendeshwa kwa njia ya kimtandao  

Amesema mapinduzi hayo yan ne yameongeza ufanisi
kuanzia pale matumizi ya kwanza hadi ya tatu yalipofikia ambapo mapinduzi ya
kwanza yalitokea katika karne ya 18 ambapo binadamu aligundua mashine ya kuwezesha
uzalishaji kwa mara ya kwanza duniani,ya pili yalileta ugunduzi wa mafuta ya
nishati na umeme pamoja na maendeleo mengine ya kisayansi,mapinduzi ya tatu
yalianza 1950 ambapo vya tehama kama tarakishi viligundulika

Kwa upande wake mwenyekiti wa mawakili wa kujitegemea George
Njooka alisema kuwa tasnia ya sheria iangalie kwa kina juu ya bongo
bandia (Artificial Teligency) ielekezwe kwenye kuelewa ubongo wa binadamu
na kuchakata matumizi yakuwa sahihi na bora ya tehama ili kubresha utoaji haki
kwa wananchi na kutatua changamoto zinazoikabili jamii

Alisema kuwa kukua kwa bongo bandia kunaweza kuleta
maendeleo kwa utoaji wa haki nchini hivyo sekta hiyo haina budi kujizatiti na
kujiandaa kufanya maandalizi mwananaili muda ukifika maboresho ya utoaji haki
na ushauri ya kisheria uelekezwe kwenye usahihi wa taarifa na sheria husika ili
haki ya mwananchi ionekane kufanyika kwa muda mfupi

Alihitimisha kwa kusema kuwa ili waweze kwenda kwa kasi
katika kuleta maboresho kuelekea mahakama mtandao inahitajika kuhakikisha kuwa
jamii inakubaliana na hayo ya kutegemea bongo bandia na matumizi ya tehama
katika utoaji haki sambamba na elimu ya kutosha itolewe ili mapokezi yake yawe
chanya .

Baadhi ya Majaji wakiwa katika maadhimisho ya wiki ya sheria yakiyofanyika katika Mahakama kuu kanda ya Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika Mahakama kuu kanda ya Arusha

Jaji Mfawidhi kanda ya Arusha Mosses
Mzuna ,Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya sheria  2/2/2022,

Baadhi
ya  Mawakili wa serikali pamoja na Mawakili wa kujitegemea wakiwa
katika maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika Mahakama kuu
kanda ya Arusha

Baadhi
ya wanachama wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA wakiwa
wameshiriki maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Arusha 2/2/2022
yaliyofanyika Mahakama kuu Kanda ya Arusha

 

 








viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/?p=1533
Post a Comment

Post a Comment