bilioni

JAPAN YAIPATIA TANZANIA SH. BILIONI 761.8 - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

 

Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dar es Salaam.

 

Serikali  ya
Tanzania na Japan zimesaini  mikataba
mitatu ya mkopo na msaada yenye thamani ya Yen za Japan bilioni 37.9 sawa na takriban shilingi bilioni 761.8 kwa ajili
ya kutekeleza miradi ya ukarabati wa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa
miundombinu ya maji Zanzibar na Ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili.

 

Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es Salaam, kati ya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba kwa niaba ya
Serikali ya Tanzania na Balozi
wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto pamoja na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan, Bw. Naofumi Yamamura, kwa naiaba ya
Serikali ya Japan.

 

Akizungumza katika hafla fupi
ya kusaini mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa Mradi wa ukarabati wa Bandari
ya Kigoma utatekelezwa kwa msaada wa Yen
za Japan bilioni 2.73 sawa na takriban shilingi bilioni 54.79, ukihusisha Ukarabati
wa gati za mashariki na kaskazini mwa Bandari ya Kigoma, ukarabati wa majengo
ya kushushia abiria na mizigo, ukarabati wa barabara zilizopo katika Bandari
hiyo na ujenzi wa majengo mapya ya abiria na mizigo.

 

“Bandari ya Kigoma ilijengwa katika kipindi cha mwaka
1912–1927 na imekuwa bandari muhimu katika kusafirisha mizigo na abiria kwenda
nchi jirani za Burundi, DR Congo, Zambia na mikoa iliyopakana na Kigoma, hivyo
kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo kutachangia kuongeza ufanisi wa
Bandari, kutoa  fursa za ajira, kupanua
wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kuchochea shughuli za kiuchumi na
kuchochea biashara kati ya Tanzania na nchi hizo jirani” alisema Bw. Tutuba

 

Alisema kuwa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji
Zanzibar, utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Yen za Japan
bilioni 10.86 sawa na takriban shilingi bilioni 218.382 ambapo mradi huo
utahusisha kujenga  na kukarabati  miundombinu ya maji Mjini Zanzibar.

 

“Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Zanzibar utaimarisha
upatikanaji wa maji kwa kudhibiti upotevu wa maji unaotokana na uchakavu wa
miundombinu ya mabomba, matangi, visima na pampu, hivyo kuwaongezea wananchi
muda wa kufanya kazi, kuondoa maradhi yanayotokana na ukosefu wa maji safi na
salama na kupunguza umasikini” alifafanua Bw. Tutuba

 

 

Bw.
Tutuba aliutaja mradi wa tatu uliopata mkopo wenye
masharti nafuu  kutoka Japan kuwa ni  Ujenzi wa Barabara ya
Arusha-Holili utakaotekelezwa
 kwa Yen za Japan bilioni 24.31 sawa na
takriban shilingi bilioni 488.667, ukihusisha pia  ujenzi wa daraja la
Kikafu  lenye urefu wa mita 560, pamoja na baadhi ya barabara
za Moshi Mjini.

 

Bw. Tutuba ameishukuru
Serikali ya Japan kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali hapa nchini ikiwa
ni utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Tatu wa Miaka Mitano pamoja
na Dira ya Mendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 na akaahidi kuwa Serikali ya
Tanzania chini ya Uongozi wa Mheshiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, itaendeleza ushirikiano na Japan kwa faida pande zote
mbili.

 

Kwa upande
wake Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, alisema kuwa amefurahia kusainiwa kwa mikataba
hiyo mitatu ukiwemo wa Barabara ya Arusha hadi Holili alioutaja kuwa ni muhimu
kwa ukuaji wa uchumi wa nchi na utachochea utangamano wa Kikanda.

 

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Japan Bw. Naofumi Yamamura, alisema kuwa Japan
imefungua milango zaidi ya kusadia maendeleo ya Tanzania na kuahidi kuwa
Shirika hilo liko tayari kupokea mapendekezo ya miradi mingine mipya ambayo
Serikali ya Tanzania itaona inafaa kupata ufadhili na mikopo nafuu.

 

Katika
kipindi cha miaka 15 kuanzia mwaka 2006 hadi 2021, Japan imeipatia Tanzania
zaidi ya yen za Japan bilioni 61.9 sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.25
ambapo kati ya fedha hizo, yen za Japan zaidi ya bilioni 30.77 sawa na shilingi
bilioni 620 ni misaada, na kiasi kingine cha yen za Japan bilioni 31.13 sawa na
shilingi bilioni 628, ni mikopo yenye masharti nafuu.

 

Sekta zilizonufaika
na ufadhili wa Serikali ya Japan ni pamoja na Nishati, Kilimo, Miundombinu ya
barabara, Maji, na Mafunzo ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu kwa Watanzania
kupitia program mbalimbali kama SDGs na ABE initiatives. 

 

Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Naofumi
Yamamura, wakisaini mikataba
mitatu ya  mkopo na msaada wa shilingi
bilioni 761.8 kwa ajili ya ukarabati wa gati za Mashariki na Kaskazini mwa
Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa
barabara ya Arusha – Holili, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Balozi wa Japan
nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, wakisaini mikataba mitatu
ya mkopo na msaada yenye thamani ya shilingi bilioni 761.8 kwa ajili
ya ukarabati wa gati za Mashariki na Kaskazini
mwa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa
barabara ya Arusha – Holili, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Naofumi Yamamura, wakionesha
mikataba mitatu ya mkopo na msaada wa shilingi bilioni 761.8 kwa ajili ya ukarabati
wa gati za Mashariki na Kaskazini mwa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa
miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa barabara ya Arusha – Holili, jijini
Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe.
Shinichi Goto, wakionesha mikataba ya mkopo na msaada wa shilingi bilioni 761.8
kwa ajili ya ukarabati wa gati za Mashariki na Kaskazini mwa Bandari ya Kigoma,
uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa barabara ya Arusha –
Holili, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi
Goto, wakibadilishana hati za mikataba ya mkopo na msaada wa shilingi bilioni
761.8 kwa ajili ya ukarabati wa gati za Mashariki na Kaskazini mwa Bandari ya
Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa barabara ya
Arusha – Holili, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (katikati), akiwa katika
picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto
(kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan
(JICA), Bw. Naofumi Yamamura, baada ya kusainiwa kwa mkataba wa msaada wa
shilingi bilioni 761.8 kwa ajili ya ukarabati wa gati za Mashariki na
Kaskazini mwa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na
ujenzi wa barabara ya Arusha – Holili, jijini Dar es Salaam.

(Picha
na WFM, Dar es Salaam)

Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba akisaini mikataba mitatu ya
mkopo na msaada yenye thamani ya shilingi bilioni 761.8 kwa
ajili ya ukarabati wa gati za Mashariki na Kaskazini mwa Bandari ya
Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa barabara ya
Arusha – Holili, jijini Dar es Salaam. (Katikati) ni Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Mhe. Shinichi Goto na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la
Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Naofumi Yamamura.

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto akiteta
jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba baada ya halfa ya  kusaini
mikataba mitatu ya  mkopo na msaada wa shilingi bilioni 761.8 kwa
ajili ya ukarabati wa gati za Mashariki na Kaskazini mwa Bandari ya
Kigoma,
uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa barabara ya
Arusha –
Holili, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) akisalimiana
na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, walipokutana kwa ajili ya halfa kusaini mikataba mitatu ya mkopo na msaada wa shilingi
bilioni 761.8 kwa ajili ya ukarabati wa gati za Mashariki na Kaskazini mwa
Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na ujenzi wa
barabara ya Arusha – Holili, jijini Dar es Salaam.

 








viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/japan-yaipatia-tanzania-sh-bilioni-761-8-swahili-viuhapa-2/
Post a Comment

Post a Comment