Akili

Diamond Platnumz Akili Nyingi Sana...Sahivi Kashakusanya Kijiji Tarehe 14 Kwa Kiki ya Zuchu - Swahili Viuhapa

featured image


viuhapa

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA Swahili Viuhapa, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Mitandao ya kijamii imekuwa ‘busy’ sana na tetesi za Rais wa WCB @diamondplatnumz kutoka kimapenzi na msanii wake @officialzuchu ambazo zilianza Disemba mwaka 2021.

Juzi nikiwa katika kijiwe kimoja ghafla nikaanza kusikia mada ya Diamond kutoka kimapenzi na msanii wake Zuchu.

Si unajua siku hizi kila mtu anamiliki simu zakupangusa, basi acha tu kila mtu ana taarifa ya chochote kinachotokea tena, kila jambo wana taarifa zote tena usithubutu kutia neno kwani wao wakiona wanaamini moja kwa moja.

Basi, mazungumzo yaliendelea.

“Kwani kuna ubaya gani? Diamond kutoka na Zuchu kimapenzi, yule sio mtoto mdogo wala sio ndugu yake”aliongea mzee mwenye umri mkubwa akibishana na vijana wadogo.

Vijana hao walikuwa wana hofu kwamba Diamond atampoteza Zuchu kimuziki huku wakitolea mifano ya mastaa wengine aliotembea nao na baadae kuwaacha.

Haya mazungumzo yalinifanya nione ukubwa wa hili jambo kibiashara, muziki kuna wakati msanii hauhitaji ngoma kali pekee, mastory ya town kuhusu maisha ya mastaa yana husika sana kibiashara kama wazungu wanavyosema ‘All publicity is good publicity’.

CHAWA WALIVALIA NJUGA.

Baada ya kuona chawa promax @officialbabalevo alizungumzia sakata hilo tena kwa upande wa ku-support kinachoendelea nikasema sasa hii imeshakuwa project ya bwana mkubwa @diamondplatnumz kwa msanii wake. Pia @RommyJons @jumalokole pamoja na watu wake wengine wa karibu walianza kulibeba suala hili

Yote haya hayamaanishi kwamba hawapo kwenye mahusiano au wapo kwenye mahusiano, ni jinsi gani Diamond alivyobadilisha sakata hili kwenda kibiashara zaidi tena kwa ukubwa.

Jana wakati @officialzuchu anahojiwa Wasafi Fm kupitia MashamSham, watu zaidi ya 15000 walikuwa wanaangalia tukio hilo ‘live’ kupitia mtandao wa YouTube. Watu wa Media wanajua ilivyongumu kupata ‘live event’ ikaangaliwa na watu wengi kwa kiasi hicho huku kukiwa na matukio ya Bunge la 12 pamoja na mambo mengine.

Kwa sasa macho ya Watanzania ni tarehe 14, siku ya Valentine Day, ‘Diamond akili nyingi’ ameshafanya yake na tayari msanii wake @officialzuchu anakwenda kukusanya mamilioni.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE




viuhapa

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

https://www.swahili.viuhapa.com/diamond-platnumz-akili-nyingi-sana-sahivi-kashakusanya-kijiji-tarehe-14-kwa-kiki-ya-zuchu-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment