Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo kinajivunia ni pamoja na kusimamia Muungano wa Tanzania na kwamba kitaendelea kuhakikisha kuwa Muungano huo unadumu milele.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Februari 4, 2022 mjini Musoma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya CCM amesmea kuwa chama hicho kimepanga kutafakari mahali kilipotoka, kilipo na kinapoelekea.
Amesema kuwa yapo mambo mengi ya mafanikio ambayo yamefanywa na chama hicho huku kubwa zaidi likiwa ni suala la amani, umoja na mshikamano wa Watanzania hivyo ni wajibu wa chama hicho kuhakikisha kuwa mambo hayo yanaendelea kuwepo na kwamba Muungano imara ni mojawapo ya sababu za kuendela kuwepo kwa mambo hayo.
Amesema kuwa licha ya Muungano huo kukumbwa na changamoto kadhaa lakini bado ni imara kutokana na namna ambavyo chama hicho kimekuwa kikishughulikia kwa uharaka pale changamoto zinapotokea na kupata suluhisho.
Amesema kuwa Watanzania bado wanakihitaji chama hicho kiendelee kuongoza nchi ambapo ameeleza kuwa kutokana na mfumo wa uongozi wa chama ni vigumu kwa chama hicho kushindwa katika uchaguzi wowote utakaofanyika nchini.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 45 ya uhai wa chama hicho, CCM kimeendelea kuwa mwalimu wa demokrasia ndani na nje ya nchi huku akisema kuwa mfumo wa uteuzi wa viongozi wa nafasi mbalimbali katika chama hicho ni wa uhakika hali ambayo imekuwa ikipelekea kupatikana kwa viongozi bora kwa nyadhifa mbalimbali.
“Sote tunakumbuka mtihani tulioupata mwaka jana kwahiyo endapo CCM tungekuwa na viongozi wa kubahatisha ina maana mama Rais Samia asingeweza kuyafanya haya anayoyafanya lakini mnaona tangu alivyoingia madarakani amejipambanua ni kiongozi wa aina gani na nchi inaendelea kupata maendeleo ” amesema
Shaka amesema kuwa Chama hicho kitahakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma zote za kijamii bila ubaguzi wa aina yoyote huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vingine kuendeleza ushirikiano na chama hicho ili kuendelea kuwa na umoja wa kitaifa kwa manufaa ya Watanzania wote.
Pia amesema kuwa chama hicho pamoja na mambo mengine kinamiliki uchumi wa zaidi ya Sh1.5 trilioni uchumi ambao unakiwezesha chama kufanya mambo yake kwa uhakika na mafaniko zaidi ikilinganishwa na vyama vingine.
Maadhimisho ya miaka 45 ya CCM kitaifa yanatarajiwa kufanyika mjini Musoma kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.
Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili
soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.
Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb
The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.
Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania
Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.
vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.
Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.
https://www.swahili.viuhapa.com/ccm-yasema-inajivunia-muungano-muungwana-blog-swahili-viuhapa/
Post a Comment