BUNGE

Bunge lafungua milango kwa nafasi ya Naibu Spika - Swahili Viuhapa

featured image


viuhapa

 

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi ametangaza nafasi ya Naibu Spika wa Bunge kuwa wazi akivitaka vyama vyenye uwakilishi bungeni kuteua wagombea watakaowania nafasi hiyo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kujiuzulu kwa Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliyeteuliwa na CCM na baadaye kushinda uchaguzi wa kuongoza mhimili huo.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha bunge leo Februari 3 imesema Wabunge watafanya uchaguzi wa nafasi hiyo Ijumaa Februari 11, 2022 na kwamba vyama vyenye uwakilishi bungeni vinatakiwa kutuma majina ya wagombea wao kwa Katibu wa Bunge kabla ya saa 10 jioni ya Februari 10, 2022.

Katibu wa Bunge amesema katika taarifa hiyo kuwa, Dk Tulia alijiuzulu kwa mujibu wa ibara ya 149 (I) (C) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ibara ya 85 (3) (b) na 86 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema, uchaguzi utafanyika haraka iwezekanavyo mara kiti hicho kitakapokuwa wazi,” inasema taarifa hiyo.

Chaguzi zote katika mhimili huo zinakuja kufuatia kujihuzuru kwa aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai Januari 6, 2022 na mchakato ukaanza kwenye vyama vya siasa.

Tofauti na uchaguzi wa Spika ambao anaweza kugombea mtu kutoka nje ya bunge, sheria inaelekeza nafasi ya Naibu Spika lazima itokane na mmoja wa wabunge.

logoblog


viuhapa

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

https://www.swahili.viuhapa.com/bunge-lafungua-milango-kwa-nafasi-ya-naibu-spika-swahili-viuhapa-2/
Post a Comment

Post a Comment