AFRIKA

Afrika Kusini yatengeneza toleo lake la chanjo ya corona ya Moderna - Swahili Viuhapa

featured image





viuhapa

 

Wanasayansi nchini Afrika Kusini wametoa nakala yao ya chanjo ya Moderna Covid, hatua ambayo wanasema inaweza kusaidia kuongeza viwango vya chanjo barani Afrika.

Kwa sasa bara hili lina idadi ndogo zaidi ya watu wanaopata chanjo ya Covid.

Kampuni inayoendesha chanjo hiyo mpya – Afrigen Biologics – inasema inatumai kuanza majaribio ya kimatibabu mnamo mwezi Novemba.

Moderna hapo awali ilisema haitakubali hataza kwenye chanjo yake, ikiruhusu wanasayansi huko Cape Town kutengeneza toleo lao la chanjo.

Watafiti hao waliungwa mkono na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Petro Terblanche, mkurugenzi wa Afrigen Biologics, alisema walikuwa wanaanza kidogo, lakini wana malengo ya kuongeza kasi siku zijazo.

“Tumetumia mpangilio ambao ni sawa na chanjo ya Moderna 1273,” aliiambia BBC.

“Hii ni sehemu ya mpango wa kimataifa wa kujenga uwezo katika nchi za kipato cha chini na cha kati ili kujitegemea.”

Chanjo inayonakiliwa ni ile ya RNA iliyotengenezwa na kampuni ya Kimarekani ya Moderna.

Pfizer-BioNTech pia ilitengeneza chanjo yake kwa kutumia teknolojia hiyo hiyo.

Zilikuwa baadhi ya chanjo za kwanza za Covid kuidhinishwa kutumika kote ulimwenguni.

Aina hii ya chanjo hufundisha seli jinsi ya kutengeneza protini ambayo itasababisha mwitikio wa kinga ndani ya miili yetu, badala ya kuweka vijidudu dhaifu au visivyotumika mwilini.

Mwanasayansi mkuu wa kampuni hiyo, Dk Caryn Fenner, alitaja mafanikio hayo ” kuwa muhimu sana.”

“Inaweka uwezo mikononi mwetu kuweza kutengeneza chanjo zetu wenyewe kwa siku zijazo, kuwa tayari kwa magonjwa zaidi ya milipuko, kutoa nyenzo za majaribio ya kimatibabu katika ardhi ya Afrika na kisha kuangalia magonjwa mengine ya umuhimu barani Afrika.”

Nchi nyingi za Afrika zimechanja kikamilifu chini ya asilimia 10 ya watu wake, ikilinganishwa na asilimia 60 Amerika Kaskazini,asilimia 63 Ulaya na asilimia 61 kote Asia.

Licha ya kuwa na viwango bora zaidi barani Afrika, Afrika Kusini imechanja asilimia 27 pekee ya watu wake.

logoblog

Thanks for reading Afrika Kusini yatengeneza toleo lake la chanjo ya corona ya Moderna






viuhapa

Viuhapa – habari tanzania kwa kiswahili

soma habari mbalimbali za tanzania na ulimwenguni kote kwa kiswahili hapa swahili Viu Hapa. Visit Swahili Viuhapa soma magazeti, habari za mastaa na udaku, umbea, mziki na hadithi za chombezo.

Viuhapa – Latest News and Gossip Leaks Celeb

The latest entertainment news and celeb leak staff worldwide can be found on Viu Hapa. Visit Viuhapa today for latest showbiz and celebrity.

Jobo escort – pata wadada wanaojiuza kutoka tanzania

Pata wadada wanaojiuza kutoka karibu yako hapa tanzania. wanatoa huduma zote. wapigie uongee nao..tembelea jobo escort tanzania. Malaya warembo wamejaa. Visit joboescort today for latest showbiz and celebrity.

vesgeta – Pata website kwa bei nafuu kwa ajili ya Kampuni au biashara yako.

Vesgeta Tech ni watengenezaji wa website / tovuti tanzania. wanatengeneza website kwa bei nafuu zaidi…. Visit vesgeta WATENGENEZA WEBSITE TANZANIA KWA BEI NAFUU.

https://www.swahili.viuhapa.com/afrika-kusini-yatengeneza-toleo-lake-la-chanjo-ya-corona-ya-moderna-swahili-viuhapa/
Post a Comment

Post a Comment