stories

Kisa Cha Mama Mkwe Wa Mwendo Kasi


“Mpaka sasa hivi bado anaendelea kukupiga?” Mama John alimuuliza mkwe wake.” Ndiyo mama tena amezidi, yaani kila siku nimekuwa kama ngoma, nimechoka Mama nibora nirudi kwetu, kwetu sijaua Mama..” Anna alaiongea huku akitokwa na machaozi. Mama mkwe wake alimuangalia kwa huruma, kisha akamuambia.

“Usiondoke mwanangu, nitaongea naye…”

“Haitasaidia chochote Mama, mara ngapi tumekaa vikao kuongea naye lakini habadiliki. Wanangu wameshakuwa wakubwa naondoka, sitaki kuendelea kuteseka…”

“Hapana usiondoke mwanangu, sasa hivi nilazima akusikilize…”. Anna alikuwa amekata tama, miaka nane ya ndoa yake ilikuwa ya mateso sana na mara kadhaa alishamlalamikia mama mkwe wake kuhusu tabia ya mumewe kumpiga lakini haikusaidia.

Kila mara mumewe alisema atajirekebisha anapokuwa mbele ya wazazi wake lakini akifika nyumbani huanza upya akimpiga  hata kwa kushitaki. Anna alishafanya mamauzi ya kuachana na mumewe, tayari alishapata chumba chake na alienda kumpa tu taarifa Mama mkwe wake ambaye walikuwa wakipatana sana.

“Wewe nenda nyumbani nitakuja huko huko kuongea naya, safari hii atanisikiliza, si bado mnafuga Kuku?” Mama mkwe wake alimuuliza swali ambalo hakuelewa kuwa lilikuwa linahusiana na nini na kupigwa kwake, lakini alijibu. “Ndiyo Mama bado tunafuga…”

Alijibu na Mama mkwe wake alimuambia kwenda nyumbani kwake na kesho yake angeenda kuwatembelea. Anna aliondoka akiwa na wasiwasi, wazo la kumuacha mumewe lilikuwa palepale, hakuwaza ni kitu gani ambacho angefanya ambacho kingemfanya kubadilisha mawazo yake.

*

Jioni ya siku iliyofuata Mama John alifika nyumbani kwa mwanae, John alikua bado hajatoka kazini na Anna alikuwa akijiandaa kupika chakula cha usiku, Mama John alimuambia mkwe wake siku hiyo anataka kupika yeye. Ingawa Anna hakutaka lakini alilazimishia mpaka akawa hana namna, aliingia jikoni na kuanza kupika akiwaambia watu wote kukaa sebuleni kuangalia TV.

John aliporejea alimkuta mkewe na watoto wakiangalia TV aliambiwa Mama yake yupo na yuko jikoni anapika, alitaka kufoka kwanini mkewe anamufanyisha kazi Mama yake ambaye alikuwa mzee lakini Mama yake alitokea na kumuambia yeye ndiyo kaamua kupika.

John alikuwa ampole kwani pamoja na ukali wake kwa mkewe lakini bado alimpenda na kumuogopa Mama yake kama mtoto. Alikaa kistaarabu sebuleni kama mkewe, Mama yake alimaliza kupika na kutenga chakula mezani, Anna na Mfanyakazi wa ndani walipotaka kumsaidia alikataa na kusema atafanya kila kitu mwenyewe.

Alitenga chakula mezani na kumpakulia kila mtu kwenye sahani kisha akawakaribisha. Ingawa haukua utaratibu kwa maana kila alikuwa akipakua chakula chake mwenyewe lakini hakuna aliyeongea, wote walifurahia chakula cha Mama.

Wakiwa wamekaa mezani baada ya sala, John alichukua kijiko na kuchota chakula, alipandisha mkono wake kukiweka mdomoni lakini kabla hajafika mdomoni Mama yake ambaye alikaa pembeni yake akimuangalia alikipiga kile kijiko chakula kikamwagika.

“Acha kula hicho chakula, chukua hiki?” Mama John aliongea huku akichukua sahani iliyokuwa na chakula cha John na kumsogezea ile ya kwake. Watu wote walishangaa kwa kile kitendo lakini Mama John hakujali, aliichukua ile sahani na kijiko alichotumia John akarudi jikoni kisha baada ya muda akarudi na sahani nyingine ambayo alikula yeye.

John aliuliza nini kinaendelea lakini Mama yake alifoka “Kula, hakuna kuongea wakati unakula! Unakuwa kama sikukufundisha nidhamu?” Mama yake alimjibu kwa sauti ya juu. Waliendelea kula  kimya kimya, hakuna aliyetaka kuongea.

*

Baada ya kumaliza kula, Mama John hakutaka mtu aguse vyombo, aliondoa vyombo mwenyewe na kuvipeleka jikoni. Kila kitu kilikuwa chakushangaza hawakujua kwanini kaamua kufanya hivyo. Baada ya kuondoa vyombo na watoto wenda kulala, ulikuwa ni wakati wa wakubwa nao kulala.

Kabla ya kwenda kulala Mama John alirudi jikoni na kuchukua sahani ya chakula, ilikuwa ni ile ambayo alimkataza mwanae kula. “Naomba mnisindikize nnje..” Aliwaambia na wao bila kujua kuwa alikua anataka kufanya nini walinyanyuka na kuongozana naye, “Uje na funguo za banda la Kuku”. Aliamrisha na Anna alienda kuchukua funguo la banda la Kuku.

Walifika katika banda la Kuku, kulikuwa na mabanda matatu, Mama John aliwaambia kufungua moja ambapo alimwaga kile chakula kwenye lile banda la Kuku ambao walianza kukimbizana, alifunga banda na kuwaambia waende wakalale. Bila kujua sababu zake za kufanya hivyo waliingia ndani kulala kila mmoja akiwa na mawazo yake.

*

Siku iliyofuata ilikua ni Alhamisi hivyo Anna na Mumewe walitakiwa kwenda kazini. Waliamka mapema na kukuta Mama mkwe kashaamka zamani na kashaandaa chai, ulikua ni mshangao kwani mara kadhaa alikuja kukaa pale na hakuwa akifanya hivyo. Aliwaandalia chai mezani na kwa mara nyingine John alipotaka kunywa alimzuia na kubadilisha kikombe.

Walimuuliza kwnaini anafanya hivyo lakini alikataa kuwajibu akiwaambia wanywe chai kwanza. Walikunywa chai na baada ya kumaliza wakati wakitaka kuondoka, aliwaambia waende kwanza kwenye banda la Kuku. Walifika na baada ya kuangalia, katika mabanda mawili hakukuwa na kitu, Kuku walikuwa salama.

Lakini katika banda lile ambalo alikua wamemwagia chakula ambalo lilikua na kuku zaidi ya kumi, wote walikuwa wamelala chini wamekufa. John na mkewe walistuka na kushangaa nini kimetokea, Mama yake aliwaangalia akiwa maetulia kwa muda kisha akasema.

“Unaona mwanangu, hicho ndiyo chakula nilichokutengea mezani jana. Nilikuwa nimeweka sumu kama ambavyo nimeweka katika chai asubuhi, kijiko kimoja tu au funda moja la chai vilitosha kukufanya kuwa kama hao Kuku hapo!” Aliongea huku akiwaangalia namna walivyokuwa wanashangaa midomo mizito hata kufunguka.

“Jana niliokoa maisha yako, lakini ningeweza kukuacha ule na subuhi ukaamka kama hao Kuku nikawaambia majirani umekufa kwa presha kama ambavyo naweza sema hawa Kuku wamekufa na kideri…

Mkeo kila siku analalamika unampiga, kila siku nakusihi acha kumpiga mkeo lakini husikii. Jana alikuja kwangu na kuniambia kuwa kachoka na anataka kuondoka, huyu ni mke mwema, wengine wanapochoka hawaondoki bali wanakuondoa wewe.

Nikuulize kitu kimoja wakati una miaka mingapi?” John alilisikia swali lakini hakuweza hata kujibu bado alikuwa ameshikwa na butwaa. “Huwezi kujibueee… mimi nakumbuka miaka 35, hembu niambie wakati unakua kuna Babu yako hata mmoja ambaye ulimuona…?

“Hapana, hata siwakumbuki…” John alijibu kinyonge kabisa.

 “Na Bibi zako…”

“Wote wapo mpaka sasa…”

“Nadhani sasa umepata jibu… chezea kila kitu lakini si mwanamke anayekupikia chakula! Usifikiri kila mwanaume anayekufa ni Mungu kapanga, wengine ni wake zao wamechoka tu kupigwa na kunyanyasika. Mke wako anaondoka kwakuwa ana kazi anajua anaweza kujihudumia, hembu jiulize kama angechoka halafu hana kazi anajua ukimuacha anaenda kuwa ombaomba…

Mimi ni Mama yako nimeona mengi, acha kujifanya mwanaume kuliko wanaume wengine, mwanaume kamili hampigi mke wake anenda kupigana na wanaume wenzake. Mimi naondoka, sitegemei kusikia umempiga mkeo tena…

Kama unataka kuendelea kumpiga basi anza kupika mwenye…” Mama John alimaliza kuongea kisha akarudi ndani akiwaacha wote wameduwaa, alichukua mfuko wake aliokuja nao na kutoka nnje kuondoka. Alirudi na kumuona mwanaea amepiga magoti akimuomba mkewe msamaha…”

Anna alikubalia kumsamehe mume wake ambaye aliahidi kutokurudia tena. John aliahidi kubadilika na kweli alibadilika, alianza kuwahi kurejea nyumbani na kurudisha mapenzi yote kama kipindi cha uchumba, hakumpiga tena mkewe na sasa ndoa yao ina miaka kumi na tano bila ugomvi wowote.

MWISHO

Post a Comment

Post a Comment