latest news

WHO: Chanjo ya corona ipo katika hatua za mwisho kutoka


Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, chanjo 70 za coronavirus ziko katika hatua ya utafiti kwenye maabara za nchi na kampuni mbalimbali duniani, huku tatu kati ya hizo zikiwa tayari zimeanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu na huenda mpaka Septemba mwaka huu ikaanza kutumika rasmi.





Wanasayansi katika maeneo mbalimbali duniani wanapambana kutengeneza kinga thabiti ya coronavirus ambayo mpaka sasa imeua zaidi ya watu 100,000 na kuathiri zaidi ya watu 1.7 milioni duniani kote huku maambukizi na vifo katika nchi kama China na Italy, yakipungua licha ya kutokuwepo na kinga.





Wataalam wa maabara wanasema kwa kawaida kinga ya coronavirus, SARS-CoV-2, inaweza kuchukua angalau mwaka hadi mwaka na nusu kukamilika na kupitishwa kuanza kutumika duniani.





Kinga hiyo inatengenezwa maalum kuzuia molecules za antigens zilizopo kwenye pathogen (virusi wanaosababisha ugonjwa), na kuongeza kinga kwenye mfumo wa mwili wa binadamu.


Post a Comment

Post a Comment