latest news

Virusi vya Corona: Wagonjwa wapya 14 waongezeka Tanzania


Wizara ya afya nchini Tanzania imetangaza kuwa kuna wagonjwa 14 wapya wa corona nchini humo.





Wagonjwa wote 14 ni raia wa Tanzania.Kufikia sasa watu 46 wameambukizwa virusi vya corona.





Watu 13 kati ya walioambukizwa viruri vya corona wapo jijini Dar es Salaam huku na mwingine mmoja kutokea mjini Arusha.





Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya Jumatatu asubuhi wagonjwa wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.





''Ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu nao unaendelea'' ilisema taarifa hiyo.





Maeneo ambayo ugonjwa huo umeripotiwa nchini Tanzania ni Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na Mwanza.



Virusi vya Corona: Jinsi marufuku ya misongamano inavyokumbana na vikwazo Afrika

Hapo jana mamlaka nchini Tanzania zilitangaza marufuku ya ndege za abiria kutua nchini humo.





Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa siku ya Jumapili na mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo (TCAA) ndege za mizigo pekee ndizo ambazo zitaruhusiwa kutua.





"Rubani na wahudumu wa ndege hizo watatakiwa kukaa kwenye karantini katika maeneo yaliyotengwa na serikali kwa gharama zao binafsi," ilisema tangazo hilo.





Hatua hiyo inakuja wakati ambapo Tanzania inakosolewa na baadhi ya wachambuzi na vyombo vya habari vya kimataifa.





Msimamo wa rais John Magufuli wa kuruhusu sehemu za ibada kuwa wazi pia unakosolewa vikali katika kipindi hiki ambacho mataifa mengi yametangaza marufuku ya mikusanyiko ikiwemo katika sehemu za ibada




Post a Comment

Post a Comment