hot news

Virusi vya Corona: Kenya yaweka rekodi mpya ya wagonjwa wengi kupona kwa siku moja

Takriban wagonjwa 15 waliokuwa wakiugua virusi vya corona nchini Kenya wamepona katika kipindi cha saa 24 zilizopita, Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mutahi Kagwe ametangaza.

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kutangazwa ncini humo na hivyobasi kufikisha idadi ya watu waliopona kwa jumla kufikia 40.

Hata hivyo watu wengine 11 wamegundulika kuwa na virusi hivyo nchini humo na kufanya idadi ya maambukizo kufikia watu 208.

Mtu mmoja pia amethibitishwa kufariki ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo kufikia watu tisa.

Kwa mujibu wa waziri Kagwe wagonjwa wapya 11 wote ni raia wa Kenya kati yaowanawake sita na wanume watano.

Wanne kati yao walikuwa wamesafiri kutoka Falme za Kiarabu (UAE) huku waliosalia wakiwa hawana historia ya kusafiri.



Kagwe aliongezea kuwa wagonjwa wanne walikuwa wanatoka kaunti ya Mandera, watatu kutoka Mombasa, Nairobi wawili huku Nakuru pamoja na Machakos wakiwa na watu mmoja mmoja.

Alisema kwamba wagonjwa wanne walikuwa wanatoka katika karantini za lazima huku saba wakipatikana kupitia usakaji wa watu waliokaribiana na wagonjwa ,alisema.

wizara ya Afya imesema kwamba jumla ya watu 2,168 waliokaribiana na wagonjwa hao walichunguzwa ambapo kati yao 1, 660 wameruhusiwa kuondoka. Hatahivyo amesema kuwa takriban watu 500 waliokaribiana na wagonjwa wa virusi hivyo wanafuatiliwa.Kagwe ametoa wito kwa Wakenya kuendelea kufuata maagizo yaliotolwa ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo

Akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi yake Kagwe amesema kwamba takriban sampuli 8000 vya watu walioko katika karantini pamoja na watu waliokaribiana nao zimefanyiwa vipimo.

Hatua zilizotangazwa na serikali ya Kenya kudhibiti coronavirus

Image captionSerikali ya Kenya imeagiza kila mtu kuvaa barakoa kila mara wawapo katika maeneo ya umma kama njia mojawapo ya kuzuwia maambuki ya virusi vya corona

Kenya ilitangaza marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa moja jioni hadi alfajiri saa kumi na moja





Marufuku ya kuingia na kutoka katika kauti nne, kaunti ya Nairobi, Kilifi na Kwale





Raia wa Kenya wameagizwa kuvaa barakoa kila mara wawapo katika maeneo ya umma





Wageni wote wanaongia nchini kutoka mataifa yaliyoathiriwa watalazimika kujitenga binaffsi kwa gharama zao.





Wakenya katika mataifa ya kigeni wametakiwa kufuata muongozo wa nchi husika





Atakayekiuka maagizo ya karantini atakamatwa kama iafisa wa ngazi ya juu wa serikali aliyetiwa mbaroni pwani ya Kenyazitasaidia serikali yake kukabili janga la corona ikiwa ni pamoja na amri ya kutotoka nje kuanzia Ijumaa Machi 27 kuanziasa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.





Kufungwa kwa baa zote na wenye hoteli kuruhusiwa tu kuuza chakula cha kwenda kula nyumbani.





Ibada za Kanisa na Swala za pamoja Misikitini zimesitishwa huku mazishi ya kiruhusiwa kuhudhuriwa na familia ya marehemu pekee.





Sherehe za harusi pia zimepigwa marufuku.




Post a Comment

Post a Comment