latest news

Corona Virus: Wajifanya mizimu kutisha watu watii amri ya kubaki majumbani Indonesia

Vijana wawili kutoka katika kijiji cha Kepuh huko nchini Indonesia wamejifanya kama mizimu kwa kuvaa vazi jeupe lililowafunika mwili mzima huku wakiweka unga mweupe usoni na kuanza kuzunguka mitaani nyakati za usiku ili kuwatisha watu wenye tabia ya kutoka nje na kutembea wakipingana na amri ya serikali ya kubaki majumbani na kuepuka kukaa makundi ili kuepusha kusambaa kwa virusi vya corona.


“Tulitaka kuwa tofauti na ndipo tukabuni njia ambayo itakuwa na athari, watu wataogopa,” amesema  Anjar Pancaningtyas kiongozi wa kikundi cha vijana ambacho kilishirikiana na polisi katika wazo hilo ili kupunguza watu kutoka nje na kutembea.


Vijana hao waliojitolea ni Deri Setyawan mwenye umri wa miaka 25, na Septian Febriyanto miaka 26, wamekuwa wakitembea katika mitaa ya Kepuh, Indonesia ikiwa ni baada kubadili mbinu za kuwatisha watu ambapo hapo awali walikuwa wakitulia tu sehemu mmoja.





Tangu kuanza kwa mtindo huo wa kutumia vijana na kujivisha uhusika kama wa nafsi za watu waliokufa mwezi huu kumeonekana kuleta mabadiliko na kumepunguza idadi ya watu kutoka nje.

Source:b5




Post a Comment

Post a Comment