celeb

Babalevo “Kusainiwa na Diamond au Alikiba ni bahati ya mtende, Wengine wamekalia kusema wao wakubwa huku mambo hayaendi kumbe ni wakongwe”


Msanii wa muziki wa bongo Fleva Babalevo ameweka wazi nia yake ya kusainiwa katika lebo mbili kubwa za muziki nchini Tanzania ambazo ni WCB iliyopo chini ya Diamond Platnumz na KINGS MUSIC iliyopo chini ya Alikiba.





Babalevo amesema kuwa ” Diamond akitaka kukusaini siwezi kukata kuingia WCB sio Diamond tu hat Alikiba ni bahati ya Mtende hiyo”





Babalevo aliongeza kuwa “kukutwa kwenye muziki sio tija shida ni kuwa na hela, Unajua kuna utofauti watu wanatakiwa wajue kuna msanii mkubwa na msanii mkongwe, kuna mtu anang’anga’nia tu mi msanii mkubwa kwa sababu tu alianza kuimba zamani, wewe ni mkongwe sasa hivi wasanii wakubwa wanajulikana, Ukitaka kutaja wasanii wakubwa utawataja ambao ni Diamond Platnumz, Alikiba, Rayvanny na Harmonize hao ndio wasanii wakubwa kwenye hii nchi wanafanya kazi kubwa zinaonekana lakini sisi wengine ni wakongwe tuna ukubwa gani vitu haviendi”




Post a Comment

Post a Comment