Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imehairisha marudio ya uchaguzi wa urais katika kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homabay kutokana na kile ilichokitaja kuwa hali mbaya ya usalama.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, ametangaza kuwa marudio hayo ya uchaguzi sasa yataandaliwa tarehe 28 mwezi huu.
Kaunti hizo ni ngome za upinzani na nyumbani kwa kinara wa upinzani Raila Odinga.
Post a Comment