videomusic

Vanessa Mdee Apiga Kolabo na Peter Okoye wa P Square..Sikiliza hapa


AKIWA amemaliza jukumu la kuigiza katika kampuni ya MTV SHUGA, mwimbaji maarufu wa kike wa Afrika Mashariki, Vanessa Mdee aka Vee Money, hivi karibuni ametoa singo inayokwenda kwa jina la Kisela.

Katika ngoma hiyo, amemshirikisha mfalme wa muziki wa pop wa Nigeria, Mr P (Peter Okoye) wa kundi la P Square. Wimbo huo wenye mvuto mkubwa unasimulia sononeko la mwanamke anayegundua kwamba kile alichofikiria kuwa uhusiano wa kweli kumbe si lolote na si chochote.


Singo hiyo iliyoongozwa na kampuni ya Clarence Peters, na kutolewa na prodyuza E Kelly (aliyewahi kutoa wimbo wa Cash Mdame wa Vanessa) ni kielelezo kingine cha umahiri wa Vanessa katika kufikisha ujumbe kwa wasikilizaji na watazamaji.

Nyota hao wawili ni kiburudisho tosha katika wimbo huo ambapo Vanessa amekaririwa akisema Peter Okoye ni alama ya muziki na kwamba kutimia kwa ushirikiano wao huo kulimpa Vanessa somo la ziada na burudani na kumwongezea sifa katika unyenyekevu na utaalam wa kazi yake.
Post a Comment

Post a Comment