Katika ulimwengu wa mitindo ata sanaa ya michoro utumika kurembesha kitu fulani ndio maana unakuta nyumba imepambwa na urembo wa picha za michoro, hata kwenye mwili ya binadamu wengine upendelea kuchora michoro tofauti kama tatoo.
Baadhi ya mastaa bongo wamechora tatoo zaidi ya moja na wengine
wakidai ukichora tatu lazima uchore nyingine na nyingine kwani
inakufanya uwe unatamani tamani, tatoo ina michoro tofauti tofauti miaka
ya 90 wengi walichora nanga pamoja na fuvu, miaka ilivyozidi kwenda
kukaja mchoro wa kappa, na sasa michoro ya maua na majina imeonekana
kupendwa zaidi.
Wanaume wengi upendelea kuchora michoro ya majina na picha kama za
siura za wazazi wao ama watoto wao au maandishi ya kitu furani.
Kwa upande wa wamawake upendelea picha za maua hasa ua rose,
upendelea nembo kama kopa(love) ama kitu fulani pia kuandika majina ama
maandishi ya kitu fulani.
Tatoo uvutia zaidi kwa mtu mwenye rangi angavu yani mweupe kuliko
mwenye rangi nyeusi kwani haitaonekana vizuri. Ila zingatia kuwa kabla
ya kuchora tatoo unaona na wataalau wa masuala ya ngozi iliusipate
madhara kama kuvimba mwili ama kutokwa na vipele.
Na Laila Sued
Post a Comment