sports

Video: Simba FC kulipeleka sakata la alama 3 za Kagera Sugar , FIFA kwa dola elfu 15


Rais wa timu ya soka ya Simba, Evance Aveva, amesema watapeleka malalamiko yao katika Shirikisho la soka duniani (FIFA) juu ya kupokonywa alama tatu za mezani walizopata baada ya Kagera Sugar kumchezaji mchezaji mwenye kadi tatu za njano.

Uamuzi wa kamati ya sheria ya TFF kuirejeshea Kagera Sugar pointi tatu limeiibua Simba na sasa imepanga kwenda Fifa kudai haki yake.

Kamati hiyo ilitoa uamuzi wake wiki iliyopita na kutengua uamuzi wa awali uliofanywa na kamati ya saa 72 ulioipa Simba pointi tatu baada ya kubaini Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo wa Simba na Kagera uliochezwa Aprili 2 mkoani Kagera.

Rais wa Simba, Evance Aveva amewaambia wanahabari leo katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi kuwa wanangojea barua kutoka bodi ya ligi kabla ya kwenda Fifa.

“Nawaomba wanachama na mashabiki watulie. Pointi tatu ni mali ya Simba, hadi sasa kamati iliyotengua uamuzi wa awali haikuwa na mamlaka hayo. Tunakwenda Fifa kudai haki yetu.

“Hatuwezi kurudi tena kamati ya saa 72, tuna mashauri yetu mengi lakini hayasikilizwi na kutolewa uamuzi ni bora twende ngazi za juu,”amesema Aveva.