health

Sehemu ya mwanamke iliyokeketwa kurudishwa -Bongo Hot



Faraja itarudi katika maisha ya wanawake waliokeketwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kurudisha eneo la nyama lililokatwa.

Hatua hiyo, itarudisha faraja kwa wanawake waliokeketwa ambao walipoteza hisia za mapenzi na maumivu ya kubezwa.

Upasuaji huo ambao upo katika hatua za majaribio ukifanikiwa kwa asilimia kubwa utawarudishia waathirika wa ukeketaji raha na hamasa ya kufanya mapenzi kwa uhuru.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa, wanawake zaidi ya milioni 133 duniani kote wamekuwa wakikabiliwa na ukeketaji.

Dr Hannes Sigurjónsson, aliyekuwa akifanya utafiti kuhusu upasuaji huo aliliambia Jarida la VICE kuwa kwa mara ya kwanza upasuaji waliofanya nchini Sweden umeleta mafanikio.

Sigurjónsson ambaye anafanyakazi  kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu  Karolinska kilichopo eneo la  Solna nchini Sweden, anasema cha kufurahisha zaidi wakati wa ukekektaji wasichana au wanawake huondolewa sehemu tu ya nyama ya eneo husika na kuacha sehemu kubwa kwa ndani ambayo ikifanyiwa kazi inaweza kuleta matokeo chanya.

“Inawezekana kufungua uke tena na kuunganisha kitu kama kofia ili kurudisha katika hali ya kawaida, upasuaji hauepukiki lazima ufanyike ili kuchimbua kilichobaki , ”anasema.

Post a Comment

Post a Comment