Unaweza kusema sasa mambo yanazidi kuamka baada ya mmoja wa wanachama maarufu wa Simba, Mohammed Dewji kuiambia Simba imlipe kiasi cha Sh bilioni 1.4 anazoidai.
Mo Dewji amewaambia Simba wamlipe mara tu baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.
Taarifa zinaeleza, Mo alikuwa akiikopesha Simba mshahara wa Sh milioni 80 kila mwezi kwa makubaliano fedha hizo zitaingizwa kwenye deni baada ya suala lake la uwekezaji kukubaliwa.
Mo aliahidi kuingiza uwekezaji wa Sh bilioni 20 ili kupata asilimia 51 za hisa za Simba.
Hata hivyo mchakato wa suala hilo ulikuwa mrefu na mwisho imeelezwa upande wa Evans Aveva waliamua kuingia mkataba na SportPesa bila ya kuwashirikisha baadhi ya wajumbe na wadau wa Simba akiwemo Mo Dewji.
Jambo hilo linaonekana kumkera Mo ambaye ametaka kulipwa fedha hizo Sh bilioni 1.4 ambazo Simba wanazitambua.
Hata hivyo, Mo Dewji hakudai fedha nyingine ambazo alikuwa akitoa kama bonus kwa wachezaji na chache ambazo alisaidia.
“Zile fedha nyingine alikuwa akisaidia na Simba wanajua. Lakini hizi za mshahara zilikuwa makubaliano wakati ukisubiriwa mchakato wa uwekezaji na deni lake lingeingizwa ndani ya klabu baada ya mfumo kukamilika,” kilieleza chanzo.
“Ni kweli Aveva hakutaka kutoa ushirikiano na hata walipoitisha kamati ya utendaji waliwasomea tu mkataba bila ya kuwaonyesha
Post a Comment