Hi ni aina ya cheni ilitoka kwenye miaka ya 90’s na ilionekana kubamba vizuri kwenye ulimwengu wa mitindo miaka hiyo.
Kwa sasa, aina hii ya cheni imerudi tena na imerudi ikiwa imeongezewa nakshi nakshi nyingine zaidi, tofauti na miaka ya zamani ambako haikuwa na urembo wa ziada.
Ukizungumzia choker kwa wapenda mavazi, hawatoshangaa jina hili na hapo watawaza nguo gani inafaa kwa aina hizi za cheni ambayo imeendelea kufanya vizuri zaidi kwa sasa.
Wabunifu mbali mbali wa mavazi nao hawabaki nyuma na wamefikiria mbinu zaidi na kwa sasa, kuamua kuleta choker za kiume, ambazo nazo zimeonekana zikivaliwa kwa kasi na vijana wanaoenda na wakati.
Choker zinampendeza zaidi mtu mwenye shingo ndefu, ila kwa mtu mwenye shingo fupi haushauriwi sana kuivaa.
Na Laila Sued