Wanafunzi zaidi ya 20 na walimu wao (idadi haijafahamika) wamefariki dunia baada ya basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Mlima Rhotia wilayani Karatu Arusha wakati wakielekea kwenye ziara ya kimasomo
Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa wanafunzi hao ni wa shule ya St. Lucky Vincent Nursery & Primary School English Medium iliyopo Arusha, walikuwa wakienda kwenye shule nyingine kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mtihani wa ujirani mwema.
Mazingira ya shule hiyo.
Inaelezwa kuwa ni watoto wanne(4) pekee ndiyo wanasadikiwa kuwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasi wasi vifo vikaongezeka kutokana na hali mbaya ya majeru wa ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha na kusema atatoa taarifa kama ajali hiyo imesababisha madhara akifika eneo la tukio.
Post a Comment