health

MAMBO 3 YANAYOFANYA MTU KUNENEPA KWA KASI


Leo tutamalizia kueleza sababu pia tutashauri vyakula vinavyosaidia kutatua tatizo hili la unene. Ungana nami. Mazoezi ya kutafuta stamina huongeza ukubwa wa nyama za misuli kitu kinachofanya mwili wako kuunguza/kutumia mafuta kwa sana na kuondoa unene au kitambi.

Homoni ya mkazo iitwayo Cortisol huongeza kiwango cha mafuta kinachochukuliwa mwilini na kutanua seli za mafuta. Uwepo wa kiwango kikubwa cha homoni hii huhusiana kwa karibu na ongezeko la mafuta mwilini.

1. USINGIZI

Kama wewe ni mmoja wa watu wale wanaokosa muda wa kutosha kulala kwa ajili ya mihangaiko ya hapa na pale unapaswa kuongeza muda wako wa kupumzika. Utafiti uliofanywa kwa miaka 16 kwa wanawake 70,000 ukachapishwa katika Jarida la Medicine and Science in Sports and Exercise ulibaini wanawake waliolala masaa matano au chini ya hapo walitarajiwa kuongezeka kilo 14 kuliko wale waliolala saa 7. Wataalamu hushauri watu wazima kulala saa saba hadi saa nane wakati wa usiku.

2.MARADHI

Ikiwa kiwango chako cha homoni ya Testosteroni kiko juu inaweza kuashiria kutokea kwa ugonjwa wa ovari (PCOS) ugonjwa utakaosababisha iwe vigumu kupunguza uzito na kuwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari. Utafiti uliochapishwa na Jarida la Medicine and Science in Sports and Exercises, ulionyesha watu waliofanya mazoezi magumu au mazito waliweza kupunguza unene au kitambi haraka zaidi kuliko waliofanya mazoezi mepesi. Mwili haumeng’enyi aina zote za mafuta kwa njia ileile.

Utafiti unaonyesha ulaji wa vyakula vyenye mafuta kama nyama na maziwa huongeza mafuta tumboni na hufanya kitambi. Wakati ulaji wa vyakula vya mafuta kama parachichi, samaki na alizeti huuweka mwili katika umbo zuri. Ingawa kula vyakula vyenye mafuta ya aina yoyote hufanya mwili kuongeza uzito na kusababisha kitambi hivyo ni vizuri kufurahia vyakula hivyo kwa kiasi.

3. UNAKULA SANA VYAKULA VILIVYOSINDIKWA VIWANDANI

Vyakula kama mkate mweupe, wali mweupe, chipsi kuku, vinywaji vyenye sukari kama soda, juisi hufanya mwili kutanuka/kunenepa. Kitambi huambatana na kunenepa au kutanuka kwa mwili, hivyo ulaji wa vyakula vya viwandani utarudisha nyuma jitihada/uwezo wako wa kupambana na kitambi.

Vyakula vya asili kama matunda, mbogamboga na nafaka isiyokobolewa ambavyo ni vya asili huufanya mwili kusinyaa na kusaidia kuzuia kitambi. Hivyo kula dona ama kwa unga wa mahindi, mtama au uwele. Kupunguza na kuondoa kitambi kunahitaji ushirikiano wa vitu mbalimbali, vyakula vyenye kutia nguvu kidogo na vyenye nyuzinyuzi kwa wingi pamoja na vyakula vyenye wanga na sukari kidogo huku ukifanya mazoezi ya kupunguza uzito. Ikiwa unene wako ni wa kurithi basi kupunguza kitambi, itakuwa ngumu sana.







SHOW YA MSAMI BABY KWENYE  FM BEACH PARTY MKOANI TANGA ITAZAME HAPA