Wasanii Roma na Moni pamoja na Producer Bin Laden na Mtu mmoja aliyetambulika kama houseboy wa mama yake J Murder wamepatikana na Taarifa Kuthibitishwa na Mtandao wa Jamii Forums.
Roma Na wenzake kwa taarifa zaidi zinasema kwasasa wapo Polisi Oysterbey kwaajili ya mahojiano na Polisi, Taarifa zaidi tutakupa hapa hapa bongohot.Com

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanaidaiwa kuwa katika kituo cha polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa taratibu za kipolisi kwakuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo. Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru.
Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.
Akiongea na waandishi wa habari mchana huu Polisi Central jijini Dar es salaam, Kamanda Sirro alisema tukio la utekwaji wa Roma na wenzake ni aina ya matukio ambayo hutokea mara kwa mara.
“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, hili la kina Roma na wenzake ni tukio kama matukio mengine yaliyokuwa ya ujambazi kwahiyo tupeni muda tupeleleze, tukifika mahali pazuri tutawaita tuwape taarifa lakini nimeona mitandao mingi inazungumza, jana nikaona wasanii wamekutana lakini nikajiuliza hivi yangekuwa haya matukio yanatokea ya uhalifu yanapotokea watu wanakutana ingekuwaje?,” alisema Sirro.
Aliongeza, “Jamani kazi hii tumepewa kwa mujibu wa Katiba na ni lazima tutimize wajibu wetu kwa hiyo tupeni muda tutakuwa na majibu mazuri katika hili,” aliongeza.
Post a Comment