love and relation

Shoga: Masaji Nayo ni Chakula cha Usiku



HEEE heeiyaa shoga yangu wa ukweee! Ni Jumanne tulivu nimekutana na wewe mpendwa wa kona yetu hii ya mashamsham, kona ya mahaba, kona ya sebuleni kama siyo chumbani, u hali gani mwenzangu? Shoga, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu anayetupenda licha ya sisi kutompendeza kutokana na mambo tunayoyafanya kwa makusudi na kutokukusudia, naamini u bukheri wa afya.

Kwa upande wangu naendelea vizuri na kazi na familia yangu haina tatizo. Shoga najua upepo wa kisiasa unavyoendelea nchini lakini kwangu mi na wewe tuongelee mambo yetu mengine, hayo tuyaweke pembeni kwani si mahala pake hapa, upo? Baada ya kusema hayo shoga yangu ngoja nirejee kwenye mada yangu ya leo inayohusiana na kuwafanyia masaji wazee wetu kwa lengo la kuwaondoa uchovu na maumivu ya mwili na wakati mwingine katika kuwaandaa kwa chakula cha usiku.

Shoga nimeamua kutiririka na mada hii lengo likiwa lilelile la kuboresha uhusiano wa kimapenzi na wazee wetu kwa sababu mambo ya mapenzi yana upana wake ati! Nasema yana upana wake kwa sababu wapo wenzetu ambao suala la kuwafanyia masaji wazee wao siyo geni na limekuwa ni utamaduni wao. Wapo ambao hawafanyi uzembe kabisa linapokuja suala la kuwakata kucha na nywele za sehemu mbalimbali waume zao na kuwaogesha kama watoto wadogo.

Ukiwaacha hao, wapo ambao wanapokuwa kwenye eneo la kujidai na waume zao, eneo la kupata kile chakula chetu cha usiku wanawadekea kadiri wawezavyo na wanapofurahishwa kima lovedavi basi hulia weee mwanzo mwisho, heee hee heeeiyaaa! Shoga, pamoja na kuelewa hayo yote leo nimeamua kuwapa darasa kama siyo somo wenzetu hawa ambao hawajui faida ya kuwafanyia masaji waume zao jambo ambalo ni muhimu sana kwa wana ndoa.

Kuna wengine hata hawajui kama masaji nayo ni sehemu ya chakula cha usiku.  Mtu asikudanganye shoga yangu! Masaji kwa wazee wetu ambao huwa bize na mihangaiko ya kutafuta shilingi ya kula watoto mchana kutwa ina umuhimu sana na kuwafanya wana ndoa kuwa karibu.

Nasema kuwa karibu kwani mzee anapomfanyia masaji mkewe halikadhalika na mke akafanya hivyo kwa ‘mista’ wake, huwa ni burudani ya aina yake na kwa taarifa yako tu, hufurahia chakula cha usiku, wee acha tu! Wee hushtuki tu shoga yangu umuhimu wa masaji, kuna baadhi ya watu wamefungua sehemu maalum za kutoa huduma hiyo na wengi wanaokwenda huko ni wanaume.

Shoga kwa nini usimfanyie wako chumbani kwako, hebu mpe raha mzee kwa kumfanyia masaji ambayo haina gharama kwani ukiacha mafuta ya ‘Wazungu’ unaweza kutengeneza mafuta ya nazi kisha ukamchua mzee mkala chakula chenu safi na nakuapia kila atakapokuwa anaenda atakuwa akikuwaza wewe tu! Kama kawaida yangu shoga, yafanyie kazi hayo mwana kwetu, usije kesho ukanipigia au kunitumia ujumbe mfupi eti umeachika mara ohhh mzee kila siku anaenda kufanyiwa masaji za kulipia akija kwako anakurukia tu, shoga angaliaaaa!!!






SHOW YA MSAMI BABY KWENYE  FM BEACH PARTY MKOANI TANGA ITAZAME HAPA