politics

MBUNGE WA TANGA MJINI AWAHAKIKISHIA MAENDELEO TANGA......Bongo Hot

Ikumbukwe nimiezi kadha imepita tangu Mh.rais wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuru kusitisha viongozi kufanya mikutano ya hadhara nakuwataka kutumia muda huo katika kutatua kero za Watanzania.

Ila Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF jijini Tanga wamesema kwakushirikiana na Wananchi watahakikisha Tanga inakuwa na maendeleo kwa kutekeleza miradi ya Maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Tanga Mjini alikhaji Mussa Mbaruku Mwishoni mwa juma kwenye mkutano wa hadha katika viwanja vya Tangamano amesema Mkutano huo nimahususi kwa kutoa shukurani zake kwa Wananchi wa jiji la hilo kwa kumchangua pamoja na Madiwani wengi kutoka chama cha CUF.

Akizungumzia Maendeleo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kulikuwa na migogoro ila kwakipindi hichi atahakikisha baadhi ya shule zinapatiwa Umeme kwakuwasaidia Wanafunzi kujifunza kwa vitendo somo la Tehama.

Na Kileo kudra

Post a Comment

Post a Comment